11. Mke mwema anahifadhi siri za mume wake

5 – Ni mwenye kuhifadhi siri za mume na khaswa zile siri zinazopitika kati yao wawili wanapokuwa chemba katika tendo la ndoa na mambo maalum yanayohusu ujumba. Kueneza siri za mume ni miongoni mwa mambo yanayomuumiza na kumkasirisha, jambo ambalo linapingana na kumtii na kumfurahisha. Isitoshe kuficha siri ni miongoni mwa sifa za wanawake wema, watiifu ambao wamesifiwa na Allaah pale aliposema:

حَافِظَاتٌ لِّلْغَيْبِ بِمَا حَفِظَ اللَّـهُ

“… wenye kujihifadhi katika hali ya kutokuweko waume zao kwa kuwa Allaah ameamrisha wajihifadhi.”[1]

Kwa sababu miongoni mwa kujihifadhi kwao waume wao wanapokuwa mbali kunaingia vilevile kutoeneza siri zao.

Asmaa´ bint Yaziyd (Radhiya Allaahu ´anhaa) amesimulia ya kwamba alikuwa kwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayh iwa sallam) wakati ambapo wanaume na wanawake walikuwa wameketi ambapo akasema:

“Huenda mwanaume akasema yale aliyofanya na mkewe na huenda mwanamke akasema yale aliyofanya na mumewe?” Wakanyamaza na hawakujibu kitu. Nikasema: “Ninaapa kwa Allaah! Wanawake hufanya na wanaume hufanya.” Akasema: “Msifanye hivo! Hivyo ni kama mfano wa shaytwaan wa kiume aliyekutana na shaytwaan wa kike njiani akamwingilia na huku watu wanatazama.”[2]

[1] 04:24

[2] Ahmad (06/456) na ina shawahidi ambazo zinaisahihisha au angalau kwa uchache kuifanya kuwa ni nzuri. Hayo yamesemwa pia na al-Albaaniy katika ”Aadaab-uz-Ziffaaf”, uk. 144.

  • Mhusika: Shaykh Muhammad Shuwmaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Swifaat-uz-Zawjah as-Swaalihah, uk. 28-29
  • Imechapishwa: 27/09/2022