42 – Abul-Husayn Muhammad bin Ahmad bin Hasnuun an-Narsiy ametukhabarisha: Muhammad bin ´Abdillaah bin al-Husayn ad-Daqqaaq ametukhabarisha: ´Abdullaah bin Muhammad bin ´Abdil-´Aziyz ametuzindua: Muhammad bin Ziyaad bin Farwah al-Baladiy ametuhadithia: Abu Shihaab ametuhadithia, kutoka kwa Twalhah, yaani Ibn Zayd, kutoka kwa Swafwaan bin ´Amr, kutoka kwa Raashid bin Sa´d: Abud-Dardaa’ amesema:

”Allaah hamfunzi mja elimu isipokuwa humkalifisha siku ya Qiyaamah mzigo wa matendo.”

43 – Abul-Faraj al-Husayn bin ´Aliy bin ´Ubayd at-Tanaajiyriy amenikhabarisha: Ahmad bin ´Aliy bin Hishaam at-Tamiyliy ametuhadithia huko Kuufah: ´Abdullaah bin Zaydaan ametuhadithia: Muhammad bin ´Abdir-Rahmaan al-Muhraziy ametuhadithia: Ayyuub bin Yahyaa amesema: Fudhwayl bin ´Iyaadhw amesema:

”Mwanachuoni haachi kuwa mjinga wa yale aliyojifunza mpaka ayatendee kazi. Anapoyatendea kazi, ndipo anakuwa mwanachuoni.”

44 – Abul-Hasan ´Aliy bin al-Qaasim bin al-Hasan ash-Shaahid ametukhabarisha huko Baswrah: Abul-Hasan ´Aliy bin Ishaaq al-Maadiraa-iy ametuhadithia: al-Mufadhdhwal bin Muhammad ametuhadithia: Ishaaq bin Ibraahiym at-Twabariy ametuhadithia: al-Fudhwayl amesema:

”Malengo ya elimu ni matendo. Elimu ndio mwongozo wa matendo.”

45 – al-Fudhwayl amesema:

”Ni lazima kwa watu kujifunza. Wakishajifunza basi ni lazima watendee kazi.”

46 – Abul-Fath Muhammad bin Ahmad bin Abiyl-Fawaaris ametukhabarisha: ´Aliy bin ´Abdillaah bin al-Mughiyrah ametuzindua: Ahmad bin Sa´iyd ad-Dimashqiy ametuhadithia: ´Abdullaah bin al-Mu´tazz amesema:

”Elimu pasi na matendo ni kama mti usio na matunda.”

47 – Amesema tena:

”Elimu ya mnafiki inakuwa kwenye maneno yake, ilihali elimu ya muumini inakuwa kwenye matendo yake.”

  • Muhusika: Imaam Abu Bakr Ahmad bin ´Aliy al-Khatwiyb al-Baghdaadiy (afk. 463)
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Iqtidhwaa’-ul-´Ilm al-´Amal, uk. 36-38
  • Imechapishwa: 12/05/2024
  • Taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy