11. Fadhilah ya tatu ya funga: Inamkinga mfungaji kutokamana na Moto


3- Swawm ni kinga. Kwa maana nyingine swawm ni ngao na sitara ambayo inamkinga mfungaji kutokamana na mambo ya upuuzi na maneno machafu. Kwa ajili hiyo amesema:

“Itapokuwa ni siku ya funga ya mmoja wenu, basi asizungumze maneno machafu wala asipige kelele.”

Pia swawm inamkinga mtu kutokamana na Moto. Imaam Ahmad amepokea kwa cheni ya wapokezi nzuri kupitia kwa Jaabir (Radhiya Allaahu ´anh) aliyesimulia kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Swawm ni kinga dhidi ya Moto anajilinda kwayo mja kutokamana na Moto.”

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majaalis Shahr Ramadhwaan, uk. 16
  • Imechapishwa: 08/04/2020