11. Dalili ya pili kwamba yule asiyeswali sio kafiri

Fungu la pili: Dalili za kijumla zinazofanywa maalum na Hadiyth zinazofahamisha kwamba asiyeswali ni kafiri. Mfano wa hilo ni maneno ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Hakuna mja anayeshuhudia ya kwamba hapana mungu wa haki isipokuwa Allaah na kwamba Muhammad ni mja na Mtume Wake isipokuwa Allaah anamharamishia Moto.”[1]

Hili ni tamko moja. Kuna matamshi kama hayo yamepokelewa kutoka kwa Abu Hurayrah, ´Ubaadah bin as-Swaamit na ´Utbaan bin Maalik (Radhiya Allaahu ´anhum).

[1] Ahmad (5/229).

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Hukm Taarik-is-Swalaah, uk. 14
  • Imechapishwa: 22/10/2016