11. Adhkaar wakati wa kuamka kutoka usingizini

70 – Hudhayfah (Radhiya Allaahu ´anh) amesimulia:

“Alikuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) anapotaka kulala husema:

بِاسْـمِكَ اللّهُـمَّ أَمـوتُ وَأَحْـيا

”Kwa jina lako, ee Allaah, ninakufa na ninakuwa hai.”

Na anapoamka kutoka usingizini husema:

الْحَمْدُ للَّهِ الَّذِي أَحْيَانَا بَعْدَ مَا أَمَاتَنَا، وَإِلَيْهِ النُّشُورُ

“Himdi zote njema anastahiki Allaah ambaye ametupa uhai baada ya kutufisha na Kwake ndiko tutafufuliwa.”[1]

Ameipokea al-Bukhaariy.

71 – al-Baraa´ (Radhiya Allaahu ´anh) amesimulia kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) anapotaka kulala husema:

اللهُمَّ بِاسْمِكَ أحْيَا وَبِاسْمِكَ أُمُوتُ

“Ee Allaah, kwa jina Lako nakuwa hai na kwa jina Lako ninakufa.”

Na anapoamka husema:

الْحَمْدُ للَّهِ الَّذِي أَحْيَانَا بَعْدَ مَا أَمَاتَنَا، وَإِلَيْهِ النُّشُورُ

“Himdi zote njema anastahiki Allaah ambaye ametupa uhai baada ya kutufisha na Kwake ndiko tutafufuliwa.”[2]

Ameipokea Muslim.

MAELEZO

Hadiyth hizi mbili zinafahamisha uwekwaji wa Shari´ah ya kusema Dhikr hii wakati wa kulala na wakati wa kuamka. Wakati wa kulala mtu aseme:

اللهُمَّ بِاسْمِكَ أحْيَا وَبِاسْمِكَ أُمُوتُ

“Ee Allaah, kwa jina Lako nakuwa hai na kwa jina Lako ninakufa.”

Maana yake ni kwamba napata uhai na kufa kutokana na jina Lako, ee Allaah, na kutokana na kukutaja.

Wakati wa kuamka aseme:

الْحَمْدُ للَّهِ الَّذِي أَحْيَانَا بَعْدَ مَا أَمَاتَنَا، وَإِلَيْهِ النُّشُورُ

“Himdi zote njema anastahiki Allaah ambaye ametupa uhai baada ya kutufisha na Kwake ndiko tutafufuliwa.”

Ameita kuamka kutoka usingizini uhai na akaita kulala kuwa ni kifo, kwa sababu kulala ni kifo kidogo. Amesema (Ta´ala):

اللَّهُ يَتَوَفَّى الْأَنفُسَ حِينَ مَوْتِهَا وَالَّتِي لَمْ تَمُتْ فِي مَنَامِهَا فَيُمْسِكُ الَّتِي قَضَى عَلَيْهَا الْمَوْتَ وَيُرْسِلُ الْأُخْرَى إِلَى أَجَلٍ مُسَمًّىَ

“Allaah anazifisha nafsi wakati wa kufa kwake na zile zisizokufa katika usingizi wake. Huzizuia zile ambazo amezihukumia mauti na huzituma nyingine mpaka katika muda maalumu uliopangwa.”[3]

[1] al-Bukhaariy (6324).

[2] al-Bukhaariy (6312) na Muslim (2711).

[3] 39:42

  • Muhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Ad´iyah wal-Adhkaar, uk. 77-78
  • Imechapishwa: 22/10/2025