Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah amesema:
Kila mwenye busara anatambua kwamba mwenye kukanusha uwepo wa Allaah juu ya ´Arshi na juu ya mbingu kwa Aayah mfano wa:
هَلْ تَعْلَمُ لَهُ سَمِيًّا
“Je, unamjua yeyote mwenye jina kama Lake?”
amekosea kosa kubwa. Mtu huyo ima ni mfichaji au ni mdanganyifu. Hakuzungumza kwa lugha ya kiarabu kilicho wazi.
Fikira hii inapelekea kwamba ingelikuwa ni bora juu ya dini ya watu kuwaacha pasi na ujumbe. Kwa sababu matokeo, kabla ya ujumbe na baada ya ujumbe, ni sawasawa kwa hali yoyote. Hakika si vyenginevyo ujumbe umewazidishia upofu na upotofu.
MAELEZO
Hakika ni kwenda majulisho ya mbali kabisa kukanusha ujuu wa Allaah juu ya viumbe na kulingana juu ya ´Arshi kwa Aayah kama:

Kwa sababu Aayah haikanushi ujuu na kulingana; inachokanusha ni kufanana na kushabihisha peke yake. Haipingi kuwepo kwa Allaah juu ya viumbe na kulingana Kwake juu ya ´Arshi kwa njia inayolingana Naye. Aayah haimkanushii Allaah kuwa na uso, mikono na sifa za dhati na sifa za matendo. Aayah haifahamishi kupinga sifa hizi kamilifu ambazo zimethibiti kwa Allaah (Jalla wa ´Alaa).
Watu hawa, kama tulivosema, wamechukua upande wa kukanusha na wakaacha upande wa kuthibitisha. Namna hii ndivo wanavokuwa wapotofu wote. Wanaamini sehemu ya Kitabu na wanakufuru sehemu nyingine. Wanachukua yale yanayoendana nao na wanayaacha yale yasiyoendana nao. Hata inapokuja katika Hadiyth za Mtume wapotofu wanachukua yale yanayoafikiana na maoni yao ijapo ni Hadiyth dhaifu na iliyotungwa. Sambamba na hilo wanaziacha Hadiyth Swahiyh na zinazopingana na maoni yao, wanazipindisha maana na kuzifasiri kinyume na tafsiri yake, ilimradi ziweze kuendana na ´Aqiydah yao. Hivi daima ndivo wanavokuwa wapotofu. Kwa ajili hiyo inapaswa kujihadhari nao na kutokana na mifumo yao ya batili. Hili halihusu majina na sifa za Allaah peke yake; linahusu mfumo wao wote wa batili. Kwa sababu kwa mujibu wao ni kwamba Allaah hakuwazungumzisha watu kwa kiarabu kilicho wazi; kama Allaah (Ta´ala) alivosema juu ya Qur-aan.
Watu hawa wameifanya Qur-aan ni kama mafumbo na kitendawili. Wanasema kuwa Qur-aan haitakiwi kufahamika kutokana na udhahiri wake na kwamba iko na tafsiri iliyojificha, ambayo hawaifahamu isipokuwa tu wale wenye busara. Wameifanya Qur-aan kama kwamba ni mafumbo na kitendawili. Allaah (Jalla wa ´Alaa) ameifanya Qur-aan kuwa ni ubainifu, mwongozo, ponyo na shifaa kwa watu. Wao wanadai kuwa Qur-aan haifahamiki kutokana na udhahiri wake na kwamba ina maana ambayo hawaifahamu isipokuwa tu wale watu wenye busara. Wanasema uwongo katika hili. Himdi zote njema anastahiki Allaah kwamba Qur-aan iko wazi na ni nyepesi:
وَلَقَدْ يَسَّرْنَا الْقُرْآنَ لِلذِّكْرِ فَهَلْ مِن مُّدَّكِرٍ
“Kwa hakika Tumeiwepesisha Qur-aan kwa kuikumbuka, je, yuko yeyote mwenye kuwaidhika?”[1]
Ananufaika nayo mtu wa kawaida na mwanazuoni. Kila anayeisikia Qur-aan ananufaika nayo kwa kile kiwango alichomtunuku Allaah.
Ingelikuwa akili na fikira zinatosha, basi watu wasingelikuwa na haja ya ujumbe wa kiungu. Bali hakuna kilichowazidishia ujumbe wa kiungu isipokuwa tu kukorogeka zaidi, kwa sababu umekuja kwa mafumbo na kitendawili, ambayo hayafahamiki kwa udhahiri wake. Kwa mujibu wao ni kwamba ingelikuwa bora kwa watu kusalimika na Qur-aan. Kwa sababu marejeo yao ni yaleyale kabla na baada ya kutumilizwa Mtume; nayo ni akili. Kwa hivyo hawakuwa na haja ya ujumbe wa kiungu, kwa sababu hakuna ulichowazidishia isipokuwa tu upofu na kuwapotosha zaidi. Kwa vile wanaona kuwa ujumbe wa kiungu unapingana na akili, basi si vyengine isipokuwa ni upotofu.
[1] 54:17
- Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
- Mfasiri: Firqatunnajia.com
- Marejeo: at-Ta´liyqaat at-Tawdhwiyhiyyah ´alaa Muqaddimat-il-Fatwaa al-Hamawiyyah, uk. 160-162
- Imechapishwa: 09/09/2024

Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
Mfasiri: Firqatunnajia.com
Marejeo: at-Ta´liyqaat at-Tawdhwiyhiyyah ´alaa Muqaddimat-il-Fatwaa al-Hamawiyyah, uk. 160-162
Imechapishwa: 09/09/2024
https://firqatunnajia.com/109-namna-hii-ndivo-wanavokuwa-wapotofu/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)