109. Mahimizo ya Dhikr baada ya kumaliza kuswali

Dhikr za baada ya swalah tano zimeamrishwa na Allaah ndani ya Quar-aan na Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akazihimiza. Allaah (Ta´ala) amesema:

فَإِذَا قَضَيْتُمُ الصَّلَاةَ فَاذْكُرُوا اللَّـهَ قِيَامًا وَقُعُودًا وَعَلَىٰ جُنُوبِكُمْ

“Mtakapomaliza swalah, basi mdhukuruni Allaah msimamapo na mkaapo na mnapolala ubavuni mwenu.”[1]

Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa anapomaliza kuswali husema:

أستغفر الله، أستغفر الله، أستغفر الله، اللهم أنت السلام، ومنك السلام، تباركت يا ذا الجلال والإكرام

”Namuomba Allaah msamaha. Namuomba Allaah msamaha. Namuomba Allaah msamaha. Ee Allaah! Hakika wewe ndiye as-Salaam. Amani inatoka Kwako. umebarikika, Ee Mwenye utukufu na ukarimu.”

Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Yeyote ambaye kila baada ya swalah atasema:

سُـبْحانَ الله

”Allaah ametakasika kutokamana na mapungufu.”

 mara 33.

الحَمْـدُ لله

”Himdi zote njema anastahiki Allaah.”

mara 33.

واللهُ أكْـبَر

”Allaah ni mkubwa.”

mara 33.

jumla itakuwa mara tisini na tisa. Akamilishe mia kwa kusema:

لا إله إلا الله وحده لا شريك له له الملك وله الحمد وهو على كل شيء قدير

“Hapana mwabudiwa wa haki isipokuwa Allaah, hali ya kuwa peke yake hana mshirika. Ufalme ni Wake Yeye na himdi zote ni Zake Yeye Naye juu ya kila jambo ni muweza.”,

atasamehewa makosa yake hata kama yatakuwa kama povu la bahari.”

Ameipokea Muslim.

[1] 04:103

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majaalis Shahr Ramadhwaan, uk. 229
  • Imechapishwa: 04/04/2024