108. Jahmiyyah na Mu´tazilah ndio wana ´Aqiydah hiyo

115 – ´Abdur-Rahmaan bin Muhammad bin Habiyb bin Abiy Habiyb amesimulia kutoka kwa baba yake, kutoka kwa baba yake, ambaye ameeleza:

”Nilimshuhudia Khaalid bin ´Abdillaah al-Qasriy akisema siku ya Adhwhaa: “Rejeeni na mchinje! Allaah akubali vichinjwa vyenu! Mimi namchinja al-Ja´d bin Dirham. Kwani anadai kwamba Allaah hakuzungumza na Muusa maneno ya kihakika na wala hakumfanya Ibraahiym kuwa kipenzi wa karibu – Allaah ametakasika kutokana na yale anayosema al-Ja´d bin Dirham!” Halafu akashuka kwenye mimbari na kumchinja.”[1]

Jahmiyyah na Mu´tazilah wana ´Aqiydah hiyo, wanayapotosha maandiko ya Wahy juu ya maudhui hiyo na kudai kuwa Mola ametakasika na hayo yaliyotajwa hapo juu.

116 – Nimesoma katika  kitabu ”ar-Radd ´alaal-Jahmiyyah” cha ´Abdur-Rahmaan bin Abiy Haatim: ´Iysaa bin Abiy ´Imraan ar-Ramliy ametuhadithia: Ayyuub bin Suwayd ametuhadithia, kutoka kwa as-Sarriy bin Yahyaa, ambaye amesema:

”Khaalid al-Qaswriy alitutolea Khutbah na akasema: ”Rejeeni katika vichinjwa vyenu – Allaah awakubalie! Hakika namchinja al-Ja´d… ”[2]

[1] Ameipokea al-Bukhaariy katika “Khalqu Af´aal-il-´Ibaad”, uk. 69, na ad-Daarimiy katika “ar-Radd ´alaal-Jahmiyyah”, uk. 7 na uk. 133-114. Wasimulizi wake  ni wenye kuaminika isipokuwa ´Abdur-Rahmaan bin Muhammad bin Habiyb bin Abiy Habiyb, baba yake na baba yake. Mtunzi amesema:

”Hawatambuliki.” (Miyzaan-ul-I´tidaal)

Hata hivyo inatiwa nguvu na upokezi unaofuata ambao cheni yake ya wapokezi ni bora. Kwa ajili hiyo pengine ndio sababu wanazuoni wanathibitisha kisa hiki. Mtunzi amesema katika wasifu wa al-Ja´d:

”Alikuwa akiishi kati ya wanafunzi wa Maswahabah na alikuwa ni mzushi na mpotofu. Alidai kuwa Allaah hakumfanya Ibraahiym kuwa ni kipenzi Wake wa hali ya juu  na wala hakumzungumzisha Muusa. Akauliwa kutokana na sababu hiyo siku ya Kuchinja. Kisa kinatambulika.” (Miyzaan-ul-I´tidaal)

Haafidhw Ibn Hajar ametaja hayohayo katika ”Lisaan-ul-Miyzaan”.

[2] Wapokezi wa cheni ya wapokezi ni madhubuti isipokuwa bwana huyu ´Iysaa. Ibn Abiy Haatim amesema:

”Nimeandika kutoka kwake Ramlah. Baba yangu akazitazama Hadiyth zake na kusema: ”Hadiyth zake zinafahamisha kwamba si mkweli.” Kwa ajili hiyo nikaacha kuandika kutoka kwake.” (al-Jarh wat-Ta´diyl (3/1/284))

Huenda kisa hiki ni upokezi kutoka kwake, kwa sababu sio Hadiyth ya kinabii – na Allaah ndiye mjuzi zaidi.

  • Mhusika: Imaam Shams-ud-Diyn Muhammad bin Ahmad adh-Dhahabiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-´Uluww lil-´Aliy al-Ghaffaar, uk. 131-132
  • Imechapishwa: 14/07/2024
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy