112 – Hammaad bin Zayd amesema:
”Nimemsikia Ayyuub wakati alipowataja Mu´tazilah: ”´Aqiydah yao inazungukia kusema kwamba hakuna chochote juu ya mbingu.”
Cheni ya wapokezi iko wazi kama jua na imara zaidi kama nguzo kutoka bwana na mwanachuoni wa Baswrah.
113 – Muqaatil bin Hayyaan amesimulia kwamba ad-Dhwahhaak amesema kuhusiana na maneno Yake (Ta´ala):
مَا يَكُونُ مِن نَّجْوَىٰ ثَلَاثَةٍ إِلَّا هُوَ رَابِعُهُمْ وَلَا خَمْسَةٍ إِلَّا هُوَ سَادِسُهُمْ وَلَا أَدْنَىٰ مِن ذَٰلِكَ وَلَا أَكْثَرَ إِلَّا هُوَ مَعَهُمْ أَيْنَ مَا كَانُوا
“Hauwi mnong’ono wa watatu isipokuwa Yeye ni wa nne wao, na wala watano isipokuwa Yeye ni wa sita wao, na wala chini kuliko ya hivyo na wala wengi zaidi isipokuwa Yeye yupamoja nao popote watakapokuwa, kisha siku ya Qiyaamah atawajulisha yale waliyoyatenda; hakika Allaah juu ya kila jambo ni mjuzi.”[1]
“Yuko juu ya ´Arshi na hakuna kitu kinachofichikana na ujuzi Wake.”
Imekuja katika tamko jengine:
”Yuko juu ya ´Arshi na ujuzi Wake uko pamoja nao.”
Imekuja katika tamko jengine:
”Yuko juu ya ´Arshi na ujuzi Wake uko pamoja nao popote wanapokuwa.”
Ameipokea Abu Ahmad al-´Assaal, Abu ´Abdillaah bin Battwah na Abu ´Umar bin ´Abdil-Barr kwa cheni ya wapokezi nzuri. Isitoshe Muqaatil alikuwa ni imami madhubuti[2].
114 – Sadaqah amesimulia kuwa amemsikia Sulaymaan at-Taymiy amesema:
”Nikiulizwa ni Allaah yuko wapi, nasema Yuko juu ya mbingu.”[3]
Sulaymaan alikuwa ni katika maimamu wa Baswrah inapokuja katika elimu na matendo.
[1] 58:7
[2] Ameipokea pia al-Laalakaa’iy katika “Sharh Usuwl I´tiqaad Ahl-is-Sunnah wal-Jamaa´ah” (2/92 – muswada).
[3] Ameipokea al-Laalakaa’iy katika “Sharh Usuwl I´tiqaad Ahl-is-Sunnah wal-Jamaa´ah” (2/92 – muswada). Abu Shu´bah Sadaqah bin al-Muntasir ash-Sha´baaniy alikuwa hana neno, kama alivosema Abu Zur´ah, kama ilivyotajwa katika “al-Jarh wat-Ta´diyl” (2/1/434). Wapokezi waliosalia ni wenye kuaminika. al-Bukhaariy ameitaja kwa cheni ya wapokezi pungufu katika ”Khalqu Af´aal-il-´Ibaad”, uk. 71.
- Muhusika: Imaam Shams-ud-Diyn Muhammad bin Ahmad adh-Dhahabiy
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: al-´Uluww lil-´Aliy al-Ghaffaar, uk. 129-130
- Imechapishwa: 14/07/2024
- Taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
112 – Hammaad bin Zayd amesema:
”Nimemsikia Ayyuub wakati alipowataja Mu´tazilah: ”´Aqiydah yao inazungukia kusema kwamba hakuna chochote juu ya mbingu.”
Cheni ya wapokezi iko wazi kama jua na imara zaidi kama nguzo kutoka bwana na mwanachuoni wa Baswrah.
113 – Muqaatil bin Hayyaan amesimulia kwamba ad-Dhwahhaak amesema kuhusiana na maneno Yake (Ta´ala):
مَا يَكُونُ مِن نَّجْوَىٰ ثَلَاثَةٍ إِلَّا هُوَ رَابِعُهُمْ وَلَا خَمْسَةٍ إِلَّا هُوَ سَادِسُهُمْ وَلَا أَدْنَىٰ مِن ذَٰلِكَ وَلَا أَكْثَرَ إِلَّا هُوَ مَعَهُمْ أَيْنَ مَا كَانُوا
“Hauwi mnong’ono wa watatu isipokuwa Yeye ni wa nne wao, na wala watano isipokuwa Yeye ni wa sita wao, na wala chini kuliko ya hivyo na wala wengi zaidi isipokuwa Yeye yupamoja nao popote watakapokuwa, kisha siku ya Qiyaamah atawajulisha yale waliyoyatenda; hakika Allaah juu ya kila jambo ni mjuzi.”[1]
“Yuko juu ya ´Arshi na hakuna kitu kinachofichikana na ujuzi Wake.”
Imekuja katika tamko jengine:
”Yuko juu ya ´Arshi na ujuzi Wake uko pamoja nao.”
Imekuja katika tamko jengine:
”Yuko juu ya ´Arshi na ujuzi Wake uko pamoja nao popote wanapokuwa.”
Ameipokea Abu Ahmad al-´Assaal, Abu ´Abdillaah bin Battwah na Abu ´Umar bin ´Abdil-Barr kwa cheni ya wapokezi nzuri. Isitoshe Muqaatil alikuwa ni imami madhubuti[2].
114 – Sadaqah amesimulia kuwa amemsikia Sulaymaan at-Taymiy amesema:
”Nikiulizwa ni Allaah yuko wapi, nasema Yuko juu ya mbingu.”[3]
Sulaymaan alikuwa ni katika maimamu wa Baswrah inapokuja katika elimu na matendo.
[1] 58:7
[2] Ameipokea pia al-Laalakaa’iy katika “Sharh Usuwl I´tiqaad Ahl-is-Sunnah wal-Jamaa´ah” (2/92 – muswada).
[3] Ameipokea al-Laalakaa’iy katika “Sharh Usuwl I´tiqaad Ahl-is-Sunnah wal-Jamaa´ah” (2/92 – muswada). Abu Shu´bah Sadaqah bin al-Muntasir ash-Sha´baaniy alikuwa hana neno, kama alivosema Abu Zur´ah, kama ilivyotajwa katika “al-Jarh wat-Ta´diyl” (2/1/434). Wapokezi waliosalia ni wenye kuaminika. al-Bukhaariy ameitaja kwa cheni ya wapokezi pungufu katika ”Khalqu Af´aal-il-´Ibaad”, uk. 71.
Muhusika: Imaam Shams-ud-Diyn Muhammad bin Ahmad adh-Dhahabiy
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: al-´Uluww lil-´Aliy al-Ghaffaar, uk. 129-130
Imechapishwa: 14/07/2024
Taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
https://firqatunnajia.com/107-nikiulizwa-allaah-yuko-wapi/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)