Abu Ja´far at-Twahaawiy (Rahimahu Allaah) amesema:

88 –Mja anapaswa kutambua kwamba Allaah umetangulia ujuzi Wake juu ya kila kiumbe Chake.

MAELEZO

Hii ndio ngazi ya kwanza miongoni mwa ngazi za kuamini mipango na makadirio ya Allaah. Mja anatakiwa kujua na kuamini ya kwamba Allaah amejua yaliyokuwepo na yatayokuwepo kwa ujuzi Wake wa milele. Yeye ni Mwenye kusifika kwa elimu hiyo daima na milele. Ameyajua mambo yote kwa elimu Yake ilioenea kabla ya kutokea kwake. Kwa hivyo ni lazima aamini jambo hilo.

  • Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Ta´liyqaat al-Mukhtaswarah ´alaal-´Aqiydah at-Twahaawiyyah, uk. 119-120
  • Imechapishwa: 06/11/2024