106. Wakati Muusa alipoona mahali pa Allaah

110 – Mujaahid amesema kuhusiana na maneno Yake (Ta´ala):

وَنَادَيْنَاهُ مِن جَانِبِ الطُّورِ الْأَيْمَنِ وَقَرَّبْنَاهُ نَجِيًّا

”Tukamwita kutoka upande wa kulia wa mlima na Tukamkurubisha kuzungumza naye kwa siri.”[1]

”Baina ya mbingu ya saba na ´Arshi kuna pazia 70.000. Akaendelea kumsogeza karibu Muusa mpaka baina Yake na Muusa kukawa kuna pazia moja tu. Hatimaye alipoona mahali Pake na akasikia uandishi wa kalamu akasema:

قَالَ رَبِّ أَرِنِي أَنظُرْ إِلَيْكَ

“Akasema: “Mola wangu! Nionyeshe ili nikutazame.”[2]

Haya yamethibiti kutoka kwa Mujaahid, kiongozi wa tafsiri ya Qur-aan. Ameipokea al-Bayhaqiy katika ”al-Asmaa´ was-Swifaat”[3].

111 – Sufyaan amesema:

”Nilikuwa kwa Rabiy´ah bin Abiy ´Abdir-Rahmaan wakati alipoulizwa:

الرَّحْمَـٰنُ عَلَى الْعَرْشِ اسْتَوَىٰ

”Mwingi wa rehema amelingana juu ya ´Arshi.”[4]

 “Amelinagana vipi? Akajibu: “Kulingana si kitu kisichojulikana. Namna haifahamiki. Ujumbe ni wenye kutoka kwa Allaah, jukumu la Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ni kufikisha na ni wajibu kwetu kusadikisha.”

Imekuja katika tamo jengine kwamba imesihi kwamba Ibn ´Uyaynah amesema:

”Rabiy´ah aliulizwa:

الرَّحْمَـٰنُ عَلَى الْعَرْشِ اسْتَوَىٰ

”Mwingi wa rehema amelingana juu ya ´Arshi.”

”Amelingana vipi?” Akajibu: ”Kulingana si kwamba hakutambuliki. Namna haifahamiki. Ujumbe ni wenye kutoka kwa Allaah, ni jukumu la Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kufikisha na ni jukumu letu kusadikisha.”[5]

[1] 19:52

[2] 7:143

[3] Ameipokea pia Abush-Shaykh katika ”al-´Adhwamah” (1/55 och 2/49 – muswada) kwa cheni ya wapokezi Swahiyh. Wapokezi wake wote ni wenye kuaminika. Katika maelezo yake ya ”al-Asmaa´ was-Swifaat” al-Kawthariy wa Jahmiyyah amejaribu kuikejeli cheni ya wapokezi kwa Rawh bin ´Ubaadah, mtu ambaye ni madhubuti na ni mmoja katika wasimulizi wa al-Bukhaariy na Muslim, na Shibl bin ´Abbaad, ambaye ni mwenye kuaminika na ni katika wasimulizi wa al-Bukhaariy. Kitu pekee alichoweza kumponda nacho ni kwamba eti alikuwa Qadariy. Je, huko kunamjeruhi?

[4] 20:05

[5] Mtunzi ameisimulia, uk. 98, kwa cheni ya wapokezi yenye kuungana kwenda mpaka kwa Sufyaan ath-Thawriy. Ni Swahiyh. al-Laalakaa´iy ameisimulia katika “Sharh Usuwl I´tiqaad Ahl-is-Sunnah wal-jamaa´ah” (1/92) kupitia cheni ya wapokezi mwingine kutoka kwa Ibn ´Uyaynah. Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah amesema:

”Kupitia cheni ya maimamu ambao wote ni waamini, al-Khallaal amepokea kutoka kwa Sufyaan bin ´Uyaynah ambaye amesema… “ (al-Hamawiyyah, uk. 80)

  • Mhusika: Imaam Shams-ud-Diyn Muhammad bin Ahmad adh-Dhahabiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-´Uluww lil-´Aliy al-Ghaffaar, uk. 128-129
  • Imechapishwa: 14/07/2024
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy