108 – Imesuniwa kuwapa pole familia ya maiti[1]. Kuna Hadiyth mbili kuhusu hilo:
1 – Kutoka kwa Qurrah al-Muzani (Radhiya Allaahu ´anh) amesema:
“Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa akikaa, basi hukaa naye baadhi ya Maswahabah wake. Miongoni mwao alikuwa mwanaume mwenye mtoto mdogo ambaye humjia kutoka nyuma na kumketisha mbele yake. [Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akamwambia: ”Je, unampenda?” Akajibu: ”Ee Mtume wa Allaah! Allaah akupende kama ninavyompenda.”] Baada ya muda mtoto akafariki na yule baba akaacha kuhudhuria vikao kwa sababu ya huzuni ya mwanawe. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akahisi kutokuwepo kwake ambapo akasema: ”Mbona simuoni fulani?” Wakamwambia: ”Ee Mtume wa Allaah, mwanawe uliyemuona amefariki.” Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alipokutana naye akamuuliza kuhusu mtoto wake ambapo akamjibu kuwa ameaga dunia. Akamfariji. Kisha akasema: ”Ee fulani! Ni kipi kinachopendeza zaidi kwako; kuendelea kumfurahia mwanao maisha yote au kufika kesho katika moja ya milango ya Pepo na ukamkuta amekutangulia na kukufungulia mlango?” Akasema: ”Ee Mtume wa Allaah, inanipendeza zaidi yeye kunitangulia katika mlango wa Peponi ambapo akanifungulia. Akasema: ”Hilo ni lako.” [Kisha mtu mmoja wa Answaar] akasema: ”Mtume wa Allaah, Allaah anijaalie niwe fidia yako! [Hilo ni kwa ajili yake tu au ni kwa ajili yetu sote?”] Akasema: ”Bali ni kwa ajili yenu nyote.’”
Ameipokea an-Nasaaiy (1/296) na tamko ni lake, Ibn Hibbaan katika ”as-Swahiyh”, al-Haakim (1/384) na Ahmad (5/35). al-Hakim amesema:
”Cheni yake ya wapokezi ni Swahiyh.”
adh-Dhahabiy ameafikiana naye, mambo ni kama alivosema.
an-Nasaa’iy (1/264) pia amepokea kitu kama hicho, kama alivyofanya al-Bayhaqiy (4/59 na 60), isipokuwa kwamba hakutangulia kuipokea mwanzo kwa ukamilifu wake na ana nyongeza zote mpaka ya kwanza.
Hadiyth inayo nyenginezo katika ”al-Majma´” (3/10).
2 – Anas bin Maalik (Radhiya Allaahu ´anh) amesimulia ya kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Atakayemfariji ndugu yake muumini katika msiba, basi Allaah atamvika vazi la kijani atakalotukuzwa nalo siku ya Qiyaamah.” Akaulizwa: “Ee Mtume wa Allaah, kutukuzwa huko ni vipi?” Akasema: “Ni kuonewa wivu.”
Ameipokea al-Khatwiyb katika ”Taariykh Baghdaad” (7/397) Ibn ´Asaakir katika ”Taariykh Dimashq” (15/91/1). Inayo nyingine inayoitia nguvu kutoka kwa Twalhah bin ´Ubaydillaah bin Kurayz yenye cheni iliyokatika. Ameipokea Ibn Abiy Shaybah katika “al-Muswannaf” (4/164). Nayo ni Hadiyth nzuri kwa mkusanyiko wa njia zake mbili, kama nilivyobainisha hilo katika “Irwaa’-ul-Ghaliyl fiy Takhriyj Ahaadiyth Manaar-us-Sabil” na. 756.
Fahamu ya kwamba kutumia Hadiyth hizi mbili kama dalili – na khaswa ya kwanza – juu ya rambirambi ni aula zaidi kuliko kutumia kama dalili Hadiyth isemayo:
“Atakayemfariji mwenye msiba basi atapata thawabu mfano wake.”
Haijalishi kitu hata kama inatumiwa na kikosi kikubwa cha watunzi wa vitabu. Hiyo ni Hadiyth dhaifu kupitia mkusanyiko wa njia zake zote, kama alivyobainisha an-Nawawiy katika ”al-Majmuu´” (5/305), al-‘Asqalaaniy katika ”at-Talkhiysw” (5/251) na katika ”Irwaa’-ul-Ghaliyl” (757).
[1] Ni kule kuwahimiza kufanya subira kwa kuwaahidi thawabu, kumwombea du´aa maiti na aliyepatwa na msiba.
- Muhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Ahkaam-ul-Janaa-iz wa Bid´ahaa, uk. 205-206
- Imechapishwa: 29/07/2026

Muhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Ahkaam-ul-Janaa-iz wa Bid´ahaa, uk. 205-206
Imechapishwa: 29/07/2026
https://firqatunnajia.com/106-rambirambi-kwa-wafiwa/