106 – Inajuzu kumfukua maiti kaburini kwa madhumuni sahihi, kama kwa mfano akizikwa kabla ya kuoshwa au kuvikwa sanda. Hilo ni kutokana na Hadiyth ya Jaabir bin ´Abdillaah (Radhiya Allaahu ´anh) ambaye ameeleza:
”Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alimwendea ´Abdullaah bin Ubayy baada ya kuingizwa kaburini ambapo akaamuru atolewe. Akamuweka kwenye mapaja yake, akapuliza mate kutoka kinywani mwake juu yake na akamvisha kanzu yake.” [Jaabir akasema: ”Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alimswalia.] Allaah ndiye mjuzi zaidi. [Alikuwa amemvisha `Abbaas kanzu.]
Ameipokea al-Bukhaariy (3/167) kwa tamko kamili yenye ziada ya mwisho, Muslim (8/120), an-Nasaa’iy (1/284) ambaye nyongeza ya kwanza ni ya kwake, Ibn-ul-Jaaruud (260), al-Bayhaqiy (3/402) na Ahmad (3/381) kupitia kwa ´Amr bin Diynaar ambaye amesikia kutoka kwa Jaabir.
Anayo njia nyingine kutoka kwa Abuz-Zubayr kutoka kwa Jaabir:
”Alipokufa ´Abdullaah bin Ubayy basi mtoto wake alimwendea Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ambapo akasema: “Ee Mtume wa Allaah, kama hutakuja kwa ajili yake basi tutaendelea kudharauliwa kwa sababu hiyo.” Basi Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akamwendea na akamkuta tayari amewekwa ndani ya kaburi. Akasema: “Mbona hamkuniita kabla hamjaweka ndani ya kaburi?” Akatolewa, kisha Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alipuliza mate kutoka kichwani hadi miguuni na akamvisha kanzu yake.
Ameipokea Ahmad (3/371) na at-Twahaawiy katika ”al-Mushkiyl” (1/14–15) kwa cheni yenye masharti ya Muslim. Hata hivyo Abuz-Zubayr alikuwa ni mwenye kudanya hadaa na isitoshe hapa hakusema wazi amepokea kutoka kwa nani.
- Muhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Ahkaam-ul-Janaa-iz wa Bid´ahaa, uk. 202-204
- Imechapishwa: 29/07/2026

Muhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Ahkaam-ul-Janaa-iz wa Bid´ahaa, uk. 202-204
Imechapishwa: 29/07/2026
https://firqatunnajia.com/104-kumfukua-maiti-wakati-wa-dharurah/