107 – Haipendekezwi mtu kuchimba kaburi lake kabla ya kufa. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) hakufanya hivyo wala Maswahabah wake (Radhiya Allaahu ´anhum). Mja hajui atakufa wapi. Ikiwa madhumuni ya mtu ni kujiandaa kwa ajili ya mauti, basi hilo linafanywa kwa matendo mema.

Hivyo imeandikwa katika ”al-Ikhtiyaaraat al-‘Ilmiyyah” ya Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah (Rahimahu Allaah).

  • Muhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ahkaam-ul-Janaa-iz wa Bid´ahaa, uk. 204
  • Imechapishwa: 29/07/2026