106. Anachosema anayefikiwa na kitu cha kumfurahisha au kumsononesha

  Download

218-

“Alikuwa (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) anapofikiwa na kitu cha kumfurahisha basi husema:

الْحَمْـدُ للهِ الَّذي بِنِـعْمَتِهِ تَتِـمُّ الصّـالِحَات

”Himdi zote njema ni stahiki ya Allaah ambaye kwa neema Yake yanatimia mambo mema.”

Pindi anapofikiwa na kitu cha kumsononesha basi husema:

الْحَمْـدُ للهِ على كُـلِّ حاَلٍ

”Himdi zote njema ni stahiki ya Allaah kwa hali zote.”[1]

[1] Ibn-us-Sunniy katika ”‘Amal-ul-Yawm wal-Laylah” (378), al-Haakim (01/499) ambaye pia ameisahihisha. Pia ni Swahiyh kwa mujibu wa al-Albaaniy katika ”Swahiyh-ul-Jaamiy’” (04/201). Tazama ”Swahiyh Ibn Maajah” (3081).

  • Mhusika: Shaykh Sa´iyd bin ´Aliy bin Wahf al-Qahtwaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Huswn-ul-Muslim
  • Imechapishwa: 06/05/2020