Abu Ja´far at-Twahaawiy (Rahimahu Allaah) amesema:
85 – Tunaamini Ubao na Kalamu na yote yaliyoandikwa humo.
MAELEZO
Huu ni mwendelezo wa mada iliyotangulia ya kuamini mipango na makadirio. Imekwishatangulia kwamba miongoni mwa kuamini makadirio ni pamoja na kuamini yale yaliyoandikwa katika Ubao uliohifadhiwa na kwamba Allaah ameyaandika yote aliyoyajua katika Ubao uliohifadhiwa. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Kitu cha kwanza alichoumba Allaah ni kalamu. Akaiambia: “Andika!” Kukadiriwa yote yatayokuwepo hadi siku ya Qiyaamah.”[1]
Hakuna yeyote anayejua namna ulivyo Ubao na Kalamu. Ni viumbe viwili vilivyoumbwa na Allaah (´Azza wa Jall). Tunaviamini. Kwa ajili hiyo mtunzi wa kitabu amesema:
”Tunaamini Ubao na Kalamu na yote yaliyoandikwa humo.”
Bi maana Ubao uliohifadhiwa. Hii ni ngazi ya pili ya kuamini mipango na makadirio, nayo ni kuamini uandishi katika Ubao uliohifadhiwa.
[1] Ahmad (5/317), Abu Daawuud (4700) na at-Tirmidhiy (2155). Swahiyh kwa mujibu wa al-Albaaniy katika ”Dhwilaal-ul-Jannah” (1/48).
- Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: at-Ta´liyqaat al-Mukhtaswarah ´alaal-´Aqiydah at-Twahaawiyyah, uk. 116-117
- Imechapishwa: 05/11/2024
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)