Abu Ja´far at-Twahaawiy (Rahimahu Allaah) amesema:

84 – Kupinga elimu iliopo ni ukafiri na kudai elimu isiyopatikana ni ukafiri. Haithibiti imani isipokuwa kwa kukubali elimu iliopo na kuacha kutafuta elimu isiyopatikana.

MAELEZO

Upande mmoja ni ukafiri kupinga elimu ya Shari´ah na yale yote yaliyomo ndani yake katika maamrisho, makatazo na maelezo juu ya mambo yaliyopita na mambo yanayokuja huko mbele. Upande mwingine ni ukafiri kudai elimu iliyofichikana:

قُل لَّا يَعْلَمُ مَن فِي السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ الْغَيْبَ إِلَّا اللَّـهُ

“Sema: “Hakuna katika mbingu na ardhi ajuaye yaliyofichikana isipokuwa Allaah.”[1]

Kiumbe mkamilifu zaidi amesema:

وَلَوْ كُنتُ أَعْلَمُ الْغَيْبَ لَاسْتَكْثَرْتُ مِنَ الْخَيْرِ وَمَا مَسَّنِيَ السُّوءُ

“… na lau ningekuwa najua ya ghaibu, bila shaka ningelijikithirishia ya kheri na wala lisingelinigusa ovu.”[2]

Hata Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) hayajui mambo yaliyofichiakana isipokuwa yale aliyofunzwa na Allaah (´Azza wa Jall):

وَلَا يُحِيطُونَ بِشَيْءٍ مِّنْ عِلْمِهِ إِلَّا بِمَا شَاءَ

“… wala hawakizunguki chochote katika elimu Yake isipokuwa kwa akitakacho.”[3]

Haithibiti imani isipokuwa kwa kukubali elimu iliopo, nayo ni ile elimu ya Qur-aan na Sunnah, na kumuachia Allaah elimu ya mambo yenye kufichikana:

فَقُلْ إِنَّمَا الْغَيْبُ لِلَّـهِ

“Basi sema: Hakika ya ghaibu ni ya Allaah pekee.”[4]

[1]27:65

[2]7:188

[3]2:255

[4]10:20

  • Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Ta´liyqaat al-Mukhtaswarah ´alaal-´Aqiydah at-Twahaawiyyah, uk. 115-116
  • Imechapishwa: 05/11/2024