100. Ujuu wa Allaah ndani ya Tawraat

97 – Ka´b al-Ahbar amesema:

”Allaah (´Azza wa Jall) amesema ndani ya Tawraat: ”Mimi ni Allaah juu ya waja Wangu. ´Arshi Yangu iko juu ya viumbe Wangu wote. Niko juu ya ´Arshi na nayaendesha mambo ya waja Wangu. Hakuna chochote mbinguni wala ardhini kinachojificha Kwangu.”

Wapokezi wake ni madhubuti[1].

[1] Mtunzi ameisimulia kupitia kwa Abu Swafwaan al-Umawiy ´Abdullaah bin Sa´iyd bin ´Abdil-Malik bin Marwaan: Yuusuf bin Yaziyd ametuhadithia, kutoka kwa az-Zuhriy, kutoka kwa Ibn-ul-Musayyab. Cheni ya wapokezi ni Swahiyh. Wasimulizi wake ni wasimulizi wa al-Bukhaariy na Muslim. Ikiwa cheni ya wapokezi kwenda mpaka kwa Abu Swafwaan ni Swahiyh, basi Abush-Shaykh ameipokea katika “al-´Adhwamah” (2/39) kupitia kwa Nu´aym bin Hammaad, kutoka kwa Abu Swafwaan. Ni kweli kwamba Abu Nu´aym ni dhaifu, lakini inaonekana kuwa hakupwekeka kuisimulia. Kwani nimeona mtunzi anasahihisha Athar ya Ka´b katika “al-Arba´iyn fiy Swifaati Rabb-il-´Aalamiyn”,  na sioni kuwa angefanya hivo iwapo angelijua kuwa Nu´aym amepwekeka katika kuisimulia. Ibn-ul-Qayyim amesema:

”Ameipokea Abush-Shaykh, Ibn Battwah na wengineo kwa cheni ya wapokezi Swahiyh kutoka kwake.” (Ijtimaa´-ul-Juyuush al-Islaamiyyah, uk. 102)

Pengine haya yanatilia ngvuu yale niliyoyasema kwamba Athar hiyo imepokelewa kupitia njia nyingi.

  • Mhusika: Imaam Shams-ud-Diyn Muhammad bin Ahmad adh-Dhahabiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-´Uluww lil-´Aliy al-Ghaffaar, uk. 121
  • Imechapishwa: 12/07/2024
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy