Shaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (Rahimahu Allaah) amesema:

Na Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) ndiye Anajua zaidi. Swalah na amani zimfikia Mtume wetu Muhammad, kizazi chake na Maswahabah zake wote.

MAELEZO

Shaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (Rahimahu Allaah) amemalizia kitabu chake hichi kwa kurejesha elimu yote kwa Allaah (´Azza wa Jall) na kumswalia na kumsalimu Mtume Wake Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).

Hapa ndipo mwisho wa kitabu “Kashf-ush-Shubuhaat”. Tunamuomba Allaah amjaze thawabu nyingi mtunzi wa kitabu, atupe na sisi sehemu katika thawabu Zake na atukusanye sisi na yeye katika Pepo Yake; kwani hakika Yeye ni Mwingi wa kutoa na ni mkarimu. Himdi zote njema zinamstahikia Allaah, Mola wa walimwengu, na swalah na amani zimwendee Mtume wetu Muhammad.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Kashf-ish-Shubuhaat, uk. 105
  • Imechapishwa: 02/12/2023