Amesema katika dibaji yake ya kitabu “Jamaa´ah Waahidah laa Jamaa´aaat”:
“Miongoni mwa watu leo walioraddi vitabu vya Sayyid Qutwub, al-Mawduudiy, makundi ya wanaharakati, mitandao ya kivyama na Jamaa´at-ut-Tabliygh, ni ndugu yetu muheshimiwa Shaykh Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy, mjumbe wa kamati ya kufundisha katika Chuo Kikuu cha Kiislamu al-Madiynah al-Munawwarah. Hili amelifanya katika vitabu sita:
Kitabu cha kwanza: Manhaj-ul-Anbiyaa´ fiyd-Da´wah ilaa Allaah – fiyh-il-Hikmah wal-´Aql.
Kitabu cha pili: Manhaj Ahl-is-Sunnah wal-Jamaa´ah fiy Naqd-ir-Rijaal wal-Kutub wat-Twawaaif wal-Kutub.
Kitabu cha tatu: Adhwaa´ Islaamiyyah ´alaa ´Aqiydah Sayyid Qutwub.
Kitabu cha nne: Matwaa´in Sayyid Qutwub fiy Aswhaab Rasuulillaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).
Kitabu cha tano: al-Mahajjah al-Baydhwaa´ fiy Himaayat-is-Sunnah al-Ghurraa´ min Zallaat Ahl-il-Akhtwaa´ wa Zaygh Ahl-il-Ahwaa´.
Kitabu cha sita: Jamaa´ah Waahidah laa Jamaa´aat wa Swiraatw Waahid laa ´Asharaat.
Vitabu hivi – na himdi zote njema ni Zake Allaah (Ta´ala) – vimeenea ndani ya nchi na nje ya nchi. Wanafunzi wengi wamestafidi navyo, wakubwa na wadogo. Wameshuhudia ya kwamba vina malengo mazuri, ukosoaji uliosalama na maudhui yake. Ameshikamana na aina ya uandishi uliokuwa umeshikamana na wanaume waliotangulia katika maimamu wa Dini na wa uongofu ambao Allaah Amewafanya kila siku kuraddi watu wenye makosa, watu wadanganyifu na watu wa Bid´ah. Vitabu vyao sio vigeni wala vyenye kukosekana kwa watu wenye busara. Uhakikaa wa mambo ni kwamba vimeenea, vimekaguliwa na vinasomwa. Kila yule anayependa haki, anapenda Sunnah, anachukia batili na kupigana katika kutokomeza matamanio na Bid´ah, amestafidi navyo.
Kwa vile kila yule ambaye ni mwenye kufikiria nadharia fulani ni mwenye haja ya dalili juu yake, mimi napendelea kuandika misitari michache juu ya vitabu ambavyo Shaykh Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy ameandika ili kuwaonesha ndugu zetu na watoto wetu katika wale wenye inswafu ya kwamba Ruduud ambazo amepiga Shaykh Rabiy´ ni Jihaad ili kulinyanyua neno la haki liweze kuwa juu na nasaha kwa Waislamu na khaswa wale wanafunzi wapya na mfano wao wasiotilia umuhimu wowote katika ´Aqiydah mbalimbali, mifumo na Ruduud ili wasije kutumbukia katika makatazo na madhambi.”
Kisha akapiga mifano mingi ya hilo, mpaka aliposema:
“Je, yule anayezungumza kwa kuraddi mamia ya makosa haya ya khatari anafanya hivo bure au anafuata tu matamanio yake? Hapana. Bali ni katika wale ambao Allaah (´Azza wa Jalla) Amewafanya kuweza kuifanyia kazi Da´wah ya wema ya Salafiyyah. Da´wah hii imesimama katika Kitabu na Sunnah juu ya mfumo wa wema waliotangulia. Anainusuru, anaieneza na kuilinda kama jinsi mzazi anavyomlinda mwanawe au zaidi ya hivo.”
Kisha akasema:
“Hakika Shaykh Rabiy´ (Waffaqahu Allaah) amemnasihi ndugu na rafiki yake ´Abdur-Rahmaan bin ´Abdul-Khaaliq wakati alipotunga kitabu kwa jina “Jamaa´ah Waahidah laa Jamaa´aat wa Swiraatw Waahidah laa ´Asharaat”. Humo ameraddi makosa mengi ambayo Shaykh ´Abdur-Rahmaan ametumbukia ndani yake kupitia vitabu vyake na kanda zake. Radd yake juu ya makosa hayo yanatiliwa nguvu na dalili za Uteremsho na za kiakili. Shaykh Rabiy´ amenieleza, na ni mwaminifu, ya kwamba hakuandika Radd hiyo, isipokuwa baada ya kumnasihi rafiki yake ´Abdur-Rahmaan kwa kuzungumza naye na kwa kumuandikia[1]. Amesema: “Sikuona athari yoyote kwake ya kukubali nasaha wala sikuona dalili yoyote ya kuonesha kujirejea katika makosa yake ambayo ametumbukia ndani yake na kumzindua kwayo. Kwa ajili hiyo nikaandika Radd hii niliyoitaja.”
Amesema (Hafidhwahu Allaah) pia wakati alipomraddi Muhammad Suruur:
“Mimi naweza kumthibitishia Muhammad Suruur na wafuasi wake ya kwamba ikiwa Shaykh Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy, waalimu zake, marafiki zake na wanafunzi zake hawako katika mfumo wa wema waliotangulia na hawafuati Ahl-ul-Hadiyth wal-Athari, basi sijui ni yepi makusudio ya “Salafiyyah” na “Salafiyyuun”.”[2]
Amesema wakati alipokuwa akizungumzia Ruduud za Shaykh Rabiy´ kwa ´Abdur-Rahmaan ´Abdul-Khaaliq:
“Ruduud za Shaykh Rabiy´ zilikuwa ni zenye kutiliwa nguvu wanachuoni vigogo ambao wamemshuhudia Shaykh Rabiy´ kuisibu haki, upatiaji katika kukosoa na uwazi wa radd kwa kujumuisha yale yaliyoandikwa katika vitabu viwili kutokana na dalili za kinukuu na hoja za kiakili zinazoiangaza njia na kwazo hoja inasimama ju yake.”[3]
Amesema vilevile (Hafidhwahu Allaah) katika dibaji yake Radd ya Shaykh Rabiy´ kwa Hasan bin Farhaan al-Maalikiy:
“Allaah Amuwafikishe muheshimiwa na mtukufu Shaykh na ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy. Amemraddi makosa yake yote na utata wake wote wa khatari kwa dalili za Uteremsho na za kiakili kwa kuinusuru haki, nasaha kwa viumbe, kuiharibu dhuluma na kumnusuru mdhulumiwa dhidi ya mdhulumaji al-Maalikiy – na mbele ya Allaah magomvi yote yatakusanywa.
Mimi namwambia Shyakh Rabiy´ na wengine wote walio na ´Aqiydah sahihi ya as-Salafiyyah na mfumo ulionyooka, kwamba si jambo la ajabu kuona al-Maalikiy amemshambulia Shaykh mtukufu Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (Rahimahu Allaah). Mtu huyu amewasema vibaya hata Maswahabah watukufu na khaswakhaswa mtu bora katika Ummah baada ya Mtume wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), Abu Bak na wengine (Radhiya Allaahu ´anhum).
[1] Mimi mwenyewe nimeona nasaha hizi kwa hati ya mkono wa Shaykh na kadhalika nimezikopi.
[2] al-Irhaab, uk. 93.
[3] al-Irhaab, uk. 93.
- Mhusika: Shaykh Khaalid bin Dhwahwiy adh-Dhwafayriy
- Mfasiri: Firqatunnajia.com
- Marejeo: http://www.rabee.net/ar/sharticles.php?cat=12&id=57
- Imechapishwa: 04/12/2019

Mhusika: Shaykh Khaalid bin Dhwahwiy adh-Dhwafayriy
Mfasiri: Firqatunnajia.com
Marejeo: http://www.rabee.net/ar/sharticles.php?cat=12&id=57
Imechapishwa: 04/12/2019
https://firqatunnajia.com/10-shaykh-na-allaamah-zayd-bin-muhammad-bin-haadiy-al-madkhaliy-hafidhwahu-allaah/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)