11 – Muheshimiwa Shaykh ´Aliy bin Naaswir al-Faqiyhiy (Hafidhwahu Allaah)

Amesema katika kusifu kwake kitabu “Jamaa´ah Waahidah laa Jamaa´aat”:

“Nimesoma kitabu hiki na kukuta ya kwamba ni kazi ya utafiti wa kielimu na wenye kuaminika. Humo Shaykh Rabiy´ amejadiliana na Shaykh ´Abdur-Rahmaan ´Abdul-Khaaliq kwa njia ya kimaana kabisa. Kitabu hakina upetukaji mipaka na hakikutoka nje ya adabu ya Kishari´ah za kujadiliana na mazungumzo. Humo amebainisha makosa ya kimfumo ambao Shaykh ´Abdur-Rahmaan anapita juu yake katika vitabu vyake vingi na kanda zake. Ameraddi mirengo hii inayoenda kinyume na mfumo wa Salaf kwa hoja na ubainifu.”[1]

[1] Tazama dibaji ya kitabu cha Shaykh Rabiy´ ”an-Naswr al-´Aziyz”.

  • Mhusika: Shaykh Khaalid bin Dhwahwiy adh-Dhwafayriy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.rabee.net/ar/sharticles.php?cat=12&id=57
  • Imechapishwa: 04/12/2019