10. Sharti ya tisa ya wudhuu´ ni kuondoa kinachozuia kufika kwenye ngozi

Sharti ya tisa ni kuondoa chochote kinachozuia maji kufika kwenye ngozi. Lazima katika wudhuu´ maji yafike sehemu zote zinazotakiwa kufikiwa na wudhuu´. Ni lazima kuondoa kitu kinachozuia maji kufika sehemu hizo kama vile matope, unga, rangi ya kupaka au kingine chochote kinachoziba ngozi. Ama kile kinachobadilisha tu rangi ya ngozi bila kuzuia maji, kama vile hina, basi hicho hakidhuru.

  • Muhusika: ´Allaamah ´Abdul-Muhsin bin Hamad al-´Abbaad
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Shuruwt-is-Swalaah, uk. 11
  • Imechapishwa: 04/05/2026