Sharti ya nane ni kwamba maji yawe masafi na yenye kuruhusiwa. Haya ni mambo mawili. Shaykh (Rahimahu Allaah) ameyafanya kuwa sharti moja na hivyo akataja masharti kumi. Baada ya hili akataja masharti mawili zaidi. Kutokana na hilo amefanya usafi wa maji na yenye kuruhusiwa kuwa ni sharti moja.
Inashurutishwa kwamba maji ya wudhuu´ yawe ni safi. Kwa msemo mwingine ni kwamba mtu asijisafishe kwa maji yenye najisi. Pia yanapaswa yawe halali na si maji yaliyoporwa, jambo ambalo wanazuoni wametofautiana. Maoni yenye nguvu ni kwamba mtu akitawadha kwa maji yaliyoporwa, basi wudhuu´ wake ni sahihi ingawa ni mwenye dhambi kwa uporaji. Na mfano wake ni mtu anayeswali katika ardhi iliyoporwa au aliyeswali ndani ya nguo ya hariri. Mtu kama huyo swalah yake ni sahihi ingawa ni mwenye dhambi juu ya uporaji na juu ya kuvaa hariri.
- Muhusika: ´Allaamah ´Abdul-Muhsin bin Hamad al-´Abbaad
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Sharh Shuruwt-is-Swalaah, uk. 11
- Imechapishwa: 04/05/2026
Sharti ya nane ni kwamba maji yawe masafi na yenye kuruhusiwa. Haya ni mambo mawili. Shaykh (Rahimahu Allaah) ameyafanya kuwa sharti moja na hivyo akataja masharti kumi. Baada ya hili akataja masharti mawili zaidi. Kutokana na hilo amefanya usafi wa maji na yenye kuruhusiwa kuwa ni sharti moja.
Inashurutishwa kwamba maji ya wudhuu´ yawe ni safi. Kwa msemo mwingine ni kwamba mtu asijisafishe kwa maji yenye najisi. Pia yanapaswa yawe halali na si maji yaliyoporwa, jambo ambalo wanazuoni wametofautiana. Maoni yenye nguvu ni kwamba mtu akitawadha kwa maji yaliyoporwa, basi wudhuu´ wake ni sahihi ingawa ni mwenye dhambi kwa uporaji. Na mfano wake ni mtu anayeswali katika ardhi iliyoporwa au aliyeswali ndani ya nguo ya hariri. Mtu kama huyo swalah yake ni sahihi ingawa ni mwenye dhambi juu ya uporaji na juu ya kuvaa hariri.
Muhusika: ´Allaamah ´Abdul-Muhsin bin Hamad al-´Abbaad
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Sharh Shuruwt-is-Swalaah, uk. 11
Imechapishwa: 04/05/2026
https://firqatunnajia.com/09-sharti-ya-nane-ya-wudhuu-ni-maji-yawe-safi-na-halali/