10. Sababu ya sita: kufanya uadilifu baina ya watoto

Miongoni mwa sababu za familia kupata furaha ni kufanya uadilifu baina ya watoto na kutowatofautisha katika matangamano. Inatakiwa kufanya uadilifu baina yao katika tabasamu, mazungumzo, michezo na zawadi. Haya yanazikusanya nyoyo. Watoto wakiona kuwa baba yao anafanya uadilifu kati yao nyoyo zao zinakusanyika na wanakusanyika kwa baba yao. Mzazi anatakiwa kucheka, kuwazungumzisha na kucheza na wote. Kwa njia hiyo nyoyo zinakusanyika.

Akitenganisha kati ya watoto wao nyoyo zao zinatengana. Imekuja katika Hadiyth ya kwamba mwanamke wa Bashiyr bin Sa´d alimwambia mume wake: “Mpe mwanangu kijana mtumishi na umshuhudishe Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Mke alikuwa na pupa ya kumpa zawadi mvulana wake na wamshuhudishe Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). an-Nu´maan bin Bashiyr akamwendea Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na kumwambia: “Mvulana wa fulani ameniomba nimpe mvulana wake mtumishi.” Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akamuuliza: “Je, ana ndugu?” Akajibu: “Ndio.” Akamuuliza tena: “Wote umewapa mfano wa ulichompa?” Akajibu: “Hapana.” Akasema: “Si sawa kufanya hivo. Mimi sishuhudii isipokuwa haki tu.”[1] Katika upokezi mwingine alisema: “Usinishuhudishe dhuluma. Hakika watoto wako wengine pia wana haki ya kufanya uadilifu kati yao.” Abu Daawuud (3542), Ahmad (04/269) na tazama “as-Swahiyhah” (3946).

Kwa hivyo kufanya uadilifu kati ya watoto ni miongoni mwa sababu kubwa za kuifanya familia kuwa na furaha.

[1] Muslim (1624).

  • Mhusika: Shaykh Sulaymaan bin Saliymillaah ar-Ruhayliy
  • Mfasiri: Asbaab sa´aadat-il-Usrah, uk. 38-39
  • Marejeo: Firqatunnajia.com
  • Imechapishwa: 08/10/2016