10. Nasaha iliyowajibishwa kwa waislamu wote na khaswa wanachuoni

Maneno haya mafupi nimetaka kuzindua yale makosa yaliyotokea katika maneno ya mwandishi huyu kwa kuchelea baadhi ya waislamu wasije kudanganyika nayo. Hiyo ndio ile nasaha ambayo Allaah ameiwajibisha kwa waislamu na khaswa kwa wanachuoni. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Dini ni kupeana nasaha.” Tukasema: “Kwa nani, ee Mtume wa Allaah?” Akasema: “Kwa ajili ya Allaah, Kitabu Chake, Mtume Wake, viongozi wa waislamu na watu wao wa kawaida.”

Ameipokea Muslim katika “as-Swahiyh” yake.

al-Bukhaariy na Muslim wamepokea kupitia kwa Jariyr bin ´Abdillaah al-Bajaliy ambaye amesimulia kwa kusema:

“Nilikula kiapo kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) juu ya kusimamisha swalah, kutoa zakaah, kumnasihi kila muislamu na kutoka nje ya dhambi ya kuficha ambayo Allaah ametishia kwa kusema:

إِنَّ الَّذِينَ يَكْتُمُونَ مَا أَنزَلْنَا مِنَ الْبَيِّنَاتِ وَالْهُدَىٰ مِن بَعْدِ مَا بَيَّنَّاهُ لِلنَّاسِ فِي الْكِتَابِ ۙ أُولَـٰئِكَ يَلْعَنُهُمُ اللَّـهُ وَيَلْعَنُهُمُ اللَّاعِنُونَ إِلَّا الَّذِينَ تَابُوا وَأَصْلَحُوا وَبَيَّنُوا فَأُولَـٰئِكَ أَتُوبُ عَلَيْهِمْ ۚ وَأَنَا التَّوَّابُ الرَّحِيمُ

“Hakika wale wanaoficha yale Tuliyoyateremsha katika hoja za wazi na mwongozo baada ya kuwa tumeyabainisha kwa watu ndani ya Kitabu, hao anawalaani Allaah na wanalaaniwa na kila mwenye kulaani. Isipokuwa wale waliotubu na wakatengeneza na wakabainisha, basi hao nawasamehe na Mimi ni Mwingi wa kusamehe, Mwenye kurehemu.”[1]

 Namwomba Allaah (´Azza wa Jall) atuwafikishe, mwandishi na waislamu wengine wote kwua na uelewa juu ya dini yake, imara juu yake, kuipendea kheri na waja Wake na atulinde sote kutokamana na shari ya nafsi zetu, matendo yetu maovu na kuzungumza juu Yake au juu ya Mtume Wake pasi na elimu.

Swalah na salamu zimwendee Mtume wetu Muhammad, kizazi chake na Maswahabah zake wote.

[1] 02:159-160

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/articles/78/الاسلام-هو-دين-الله-ليس-له-دين-سواه
  • Imechapishwa: 11/10/2021