Huyu hapa Nabii wa mwisho kiongozi wao na bwana wa wanadamu Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Allaah amesema juu yao:

وَإِذْ يَمْكُرُ بِكَ الَّذِينَ كَفَرُوا لِيُثْبِتُوكَ أَوْ يَقْتُلُوكَ أَوْ يُخْرِجُوكَ ۚ وَيَمْكُرُونَ وَيَمْكُرُ اللَّـهُ ۖ وَاللَّـهُ خَيْرُ الْمَاكِرِينَ

“Pindi walipokupangia vitimbi wale waliokufuru ili wakufunge, au wakuue, au wakutoe [nje ya Makkah]. Na wanapanga vitimbi na Allaah anapanga vitimbi; na Allaah ni mbora wa wenye kupanga vitimbi.”[1]

وَقَالُوا يَا أَيُّهَا الَّذِي نُزِّلَ عَلَيْهِ الذِّكْرُ إِنَّكَ لَمَجْنُونٌ

”Wakasema: ”Ee ambaye umeteremshiwa Ukumbusho, hakika wewe bila shaka ni mwendawazimu.”[2]

يَقُولُونَ أَئِنَّا لَتَارِكُو آلِهَتِنَا لِشَاعِرٍ مَّجْنُونٍ

”Wanasema: ”Je, sisi kweli tuache waabudiwa wetu kwa ajili ya mshairi mwendawazimu?”[3]

Alifikwa na maudhi ya kimaneno na ya kimatendo ambayo yanatambulika kwa wanazuoni katika historia. Pamoja na hivyo akasubiri na mwisho mwema ukawa wake.

[1] 08:30

[2] 15:06

[3] 37:36-37

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Zaad Daa´iyah ila Allaah, uk. 16
  • Imechapishwa: 03/11/2021