10. Kujiandaa kwa mambo mawili kabla ya kuingia katika uwanja wa Da´wah

Shaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (Rahimahu Allaah) amesema:

Suala la nne: Kusubiri juu ya maudhi yatakayompata mtu ndani yake.

MAELEZO

Hakuna mlinganizi yeyote atakayewalingania watu katika yale waliyolingania Mitume isipokuwa atakumbana na maudhi kama jinsi maudhi yalivyowakumba Mitume na Manabii kutoka kwa watu wao. Kwa hivyo anapaswa kusubiri. Alazimiane na subira ambayo ni miongoni mwa sifa bora za watu wa imani na ni miongoni mwa akiba bora za walinganizi wanaolingania kwa Allaah (Tabaara wa Ta´ala). Ni mamoja anawalingania ndugu zake au wengineo. Anapaswa kusubiri juu ya mambo mawili:

1 – Asiingie katika uwanja wa Da´wah isipokuwa kwa subira.

2 – Akiwalingania watu na akakumbana na kitu kinachokinzana naye au anayepinga ulinganizi wake basi avumilie na aendelee katika hilo hali ya kuwa ni mwenye kumtegemea Allaah (´Azza wa Jall), akitarajia thawabu kutoka Kwake na msaada Wake. Hivo ndivo ulikuwa mwenendo wa Mitume (Swalla Allaahu ´alayhim wa sallam) wakati Allaah alipowatumiliza kuwalingania watu wao kumpwekesha Allaah (´Azza wa Jall), kuwatii, na kuwafuata Mitume Yake.

  • Mhusika: ´Allaamah Zayd bin Muhammad al-Madkhaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Twariyqal-Usuwl ilaa idhwaah-ith-Thalaat-il-Usuwl, uk. 24-25
  • Imechapishwa: 23/11/2021