Aina ya pili, nayo ni kwamba sifa hiyo imeambatana na kihusishi (إلى), imetajwa mara mbili ndani ya Qur-aan:

1 – Allaah (Ta´ala) katika Suurah al-Baqarah:

هُوَ الَّذِي خَلَقَ لَكُم مَّا فِي الْأَرْضِ جَمِيعًا ثُمَّ اسْتَوَىٰ إِلَى السَّمَاءِ فَسَوَّاهُنَّ سَبْع سَمَاوَاتٍ ۚ وَهُوَ بِكُلِّ شَيْءٍ عَلِيمٌ

”Yeye ndiye ambaye amekuumbieni vyote vilivyomo ardhini kisha kisha akazikusudia mbingu na akazifanya kamilifu mbingu saba – Naye kwa kila jambo ni Mjuzi.”[1]

2 – Amesema (Ta´ala) tena katika Suurah Fuswswilat:

ثُمَّ اسْتَوَىٰ إِلَى السَّمَاءِ وَهِيَ دُخَانٌ فَقَالَ لَهَا وَلِلْأَرْضِ ائْتِيَا طَوْعًا أَوْ كَرْهًا قَالَتَا أَتَيْنَا طَائِعِينَ

”Kisha akalingana juu ya mbingu iliali ni moshi, akaziambia pamoja na ardhi: ”Njooni kwa kutaka au kwa lazima. Zikasema: ”Tumekuja hali ya kuwa tumetii!”[2]

Kulingana maana yake ni yenye kutambulika katika lugha ya kiarabu. Hakuna mwarabu asiyejua maana ya neno hilo. Allaah amewazungumzisha waja wake ndani ya Qur-aan kwa Kiarabu kilicho wazi. Kwa mujibu wa Kiarabu kulingana maana yake ni kuwa juu na kuinuka[3].

Kwa ajili hiyo ´Aqiydah ya Salaf kuhusu Kulingana ni kumthibitishia nayo Allaah kama alivyojithibitishia nayo Mwenyewe na kama alivyomthibitishia nayo Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) pasi na kupotosha wala kukanusha, kumfanyia namna wala kumfananisha. Bali wanaamini ya kwamba Allaah amelingana juu ya ´Arshi Yake kwa namna inayolingana na utukufu na ukamilifu Wake, si kwa namna isiyofanana na kulingana na kiumbe Chake yeyote. Kwa mujibu wao Kulingana maana yake ni kuwa juu na kuinuka. Hakuna tofauti kati yao juu ya hilo. Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah (Rahimahu Allaah) amesema:

“Maneno ya Salaf, maimamu na wasimulizi wao juu ya suala hili ni mengi yanapatikana katika tafsiri za Qur-aan na vitabu vya msingi. Ishaaq bin Raahuuyah: Bishr bin ´Umar ametuhadithia:

“Nimewasikia wafasiri wengi wa Qur-aan wakisema kuhusu:

الرَّحْمَـٰنُ عَلَى الْعَرْشِ اسْتَوَىٰ

”Mwingi wa rehema amelingana juu ya ´Arshi.”[4]

”Bi maana Yuko juu ya ´Arshi.”[5]

al-Bukhaariy amesema katika ”as-Swahiyh” yake:

”Mlango wa 22:

وَكَانَ عَرْشُهُ عَلَى الْمَاءِ

“‘Arshi Yake ikawa juu ya maji.”[6]

 وَهُوَ رَبُّ الْعَرْشِ الْعَظِيمِ

”Naye ni Mola wa ‘Arshi Tukufu.”[7]

وَكَانَ عَرْشُهُ عَلَى الْمَاءِ

“‘Arshi Yake ikawa juu ya maji.”

Abul-´Aaliyah amesema:

”… kisha استوى إلى mbinguni…”

 maana yake Akawa juu:

فَسَوَّاهُنَّ سَبْعَ سَمَاوَاتٍ

“… na akazifanya kamilifu mbingu saba… ”

maana yake ni kwamba Akaziumba.”

Mujaahid amesema:

“Kwamba Yeye استوى maana yake ni kwamba Amekuwa juu ya ´Arshi.”

al-Husayn bin Mas’uud al-Baghawiy amesema katika tafsiri yake maarufu ya Qur-aan:

“Allaah (‘Azza wa Jall) amesema:

هُوَ الَّذِي خَلَقَ لَكُم مَّا فِي الْأَرْضِ جَمِيعًا ثُمَّ اسْتَوَىٰ إِلَى السَّمَاءِ فَسَوَّاهُنَّ سَبْع سَمَاوَاتٍ ۚ وَهُوَ بِكُلِّ شَيْءٍ عَلِيمٌ

“Yeye ndiye ambaye amekuumbieni yote yaliyomo ardhini kisha akazielekea mbingu na akazitimiza mbingu saba – Naye juu ya kila jambo ni Mjuzi.”[8]

Ibn ´Abbaas na wafasiri wengi wa Qur-aan wa Salaf wamesema:

”Kwa maana ya kwamba Akawa juu ya mbingu.”[9]

al-Bayhaqiy amepokea katika “al-Asmaa’ was-Swifaat”:

al-Farraa’ amesema:

”اسْتَوَى ثُمَّ maana yake ni kwamba Amekuwa juu. Ibn ´Abbaas amesema hivo. Ni kama unavyomwambia mtu: “Alikuwa amekaa, kisha اسْتَوَى na kusimama.”[10]

ash-Shaafi’iy amepokea kutoka kwa Anas (Radhiya Allaahu ‘anh) kwamba Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) amesema kuhusu siku ya ijumaa:

”Nayo ndio siku ambayo Mola wenu alikuwa juu ya ´Arshi.”[11]

Tafsiri za Qur-aan zilizopokelewa kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam), Maswahabah na wanafunzi wao, kama mfano wa tafsiri ya Qur-aan ya Muhammad bin Jariyr at-Twabariy, ´Abdur-Rahmaan bin Ibraahiym, Abu ´Abdir-Rahmaan bin Abiy Haatim, ambaye anatambulika pia kama “Duhaym” , Abu Bakr bin al-Mundhir, Abu Bakr ´Abdul-´Aziyz, Abush-Shaykh al-Aswbahaaniy, Abu Bakr bin Marduuyah na kabla ya hapo Ahmad bin Hanbal, Ishaaq bin Raahuuyah, Baqiyy bin Makhlad na kabla ya hapo ́´Abd bin Humayd, Sunayd,  ´Abdur-Razzaaq na Wakiy´ bin al-Jarraah, ndani yake kuna maneno yasiyohesabika na yanayohusiana na ya wale wanaomthibitishia Allaah sifa. Kadhalika inahusiana na vile vitabu vilivyotungwa kuhusu ´Aqiydah ambavyo ndani yake kuna mapokezi kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam), Maswahabah na wanafunzi wao.”[12]

[1] 2:29

[2] 41:11

[3] Kwa maana kwamba ikiwa neno hilo limeambatana na viambishi (على) na (إلى). Vinginevyo neno hili lina maana ya ukamilifu na utimilifu, kama ilivyo katika maneno Yake (Ta´ala):

وَلَمَّا بَلَغَ أَشُدَّهُ وَاسْتَوَىٰ آتَيْنَاهُ حُكْمًا وَعِلْمًا

“Alipofikia umri wa kupevuka na akaimarika kikamilifu… ” (28:14)

Na likitajwa pamoja na (و), maana yake ni usawa. Tazama kitabu cha Ibn-ul-Qayyim “Mukhtaswar-us-Sawaa´iq al-Mursalah”, uk. 320.

[4] 20:05

[5] al-Albaaniy amesema:

”Cheni ya wapokezi ni Swahiyh na iko na wasimulizi madhubuti na wenye kuhifadhi.” (Mukhtaswar-ul-´Uluww, uk. 160)

”Ni mmoja katika wale wenye kuhifadhi. Alikuwa ni katika rika la Ishaaq bin Raahuuyah, Ahmad bin Maniy´ na rika lao. Aliandika vitabu na alikuwa madhubuti.”

[6] 11:7

[7] 9:129

[8] 02:29

[9] Ma´aalim-ut-Tanziyl (1/59-60).

[10] al-Asmaa’ was-Swifaat (2/310).

[11] al-Musnad, uk. 70-71. adh-Dhahabiy amesema:

”Wapokezi wote hawa wanatiana nguvu – ninamuomba Allaah atujaalie ladha ya kuweza kutazama uso Wake mtukufu.” (al-´Uluww, sid. 29-30)

[12] Dar’ Ta´aarudhw-il-´Aql wan-Naql (2/20-22).

  • Muhusika: Shaykh ´Abdur-Razzaaq bin ´Allaamah ´Abdil-Muhsin al-´Abbaad al-Badr
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Athar al-Mash-huur ´an-il-Imaam Maalik fiy Swifat-il-Istiwaa’, uk. 22-24
  • Imechapishwa: 27/11/2025