Sulaymaan at-Taymiy amesema:

”Kama ningeulizwa Allaah yuko wapi, basi ningesema kuwa yupo juu ya mbingu.”

Swahiyh.

Shurayh bin ´Ubayd alikuwa akisema:

”Umeinuka Kwako mlio wa matakaso. Umepanda Kwako utulivu wa utakatifu. Utakasifu ni Wako, ee Mwenye Ukuu. Mikononi Mwako ipo mamlaka, falme, funguo na makadirio.”

Ameipokea Abush-Shaykh.

Wakati Jariyr bin al-Khatwafiy alipotaka kumsifia ´Abdul-Malik bin Marwaan alimwambia:

“Ni nini kilichokuleta, ee Jariyr?” Akasema:

Amenileta kwako Allaah Aliye juu ya ´Arshi Yake

 – na nuru na Uislamu vinakushuhudia

Ismaa´iyl bin Abiy Khaalid ameeleza kutoka kwa Abiy ´Iysaa (Rahimahu Allaah) ambaye amesema:

”Wakati Mola alipolingana juu ya Kursiy Yake kuna Malaika mmoja ambaye alisujudu. Hakunyanyua kichwa chake wala hatakinyanyua mpaka Siku ya Qiyaamah. Siku ya Qiyaamah atasema: “Sikukuabudu vile ipasavyo.”

Ameipokea Ibn-ul-Mubaarak katika ”az-Zuhd” na Abush-Shaykh katika ”al-´Adhwamah”.

Mujaahid amesema kuhusiana na maneno Yake (Ta´ala):

وَنَادَيْنَاهُ مِن جَانِبِ الطُّورِ الْأَيْمَنِ وَقَرَّبْنَاهُ نَجِيًّا

”Tukamwita kutoka upande wa kulia wa mlima na Tukamkurubisha kuzungumza naye kwa siri.”[1]

”Baina ya mbingu ya saba na ´Arshi kuna pazia 70.000. Akaendelea kumsogeza karibu Muusa mpaka baina Yake na Muusa kukawa kuna pazia moja tu. Hatimaye alipoona mahali Pake na akasikia uandishi wa kalamu akasema:

رَبِّ أَرِنِي أَنظُرْ إِلَيْكَ

“Mola wangu! Nionyeshe ili nikutazame.”[2][3]

Ameipokea al-Bayhaqiy.

Rabiy´ah amesema:

”Kulingana juu kunatambulika. Namna haitambuliki. Ujumbe ni wenye kutoka kwa Allaah, ni juu ya Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) kufikisha na ni juu yetu kuamini.”[4]

Muhayswin aliisoma Aayah namna hii:

وَفِي السَّمَاء رازِقُكُم وَمَا تُوعَدُونَ

”Juu ya mbingu yuko Mruzuku Wenu na yale mnayoahidiwa.”[5]

Hammaad bin Zayd amesema:

”Nimemsikia Ayyuub as-Sikhtiyaaniy wakati alipowataja Mu´tazilah: ”´Aqiydah yao inazungukia kusema kwamba hakuna chochote juu ya mbingu.”[6]

Ameipokea at-Twabaaraniy katika ”as-Sunan”.

al-Awzaa´iy amesema:

”Tulikuwa wakati ambao wanafunzi wa Maswahabah wamejaa tukisema: ”Hakika Allaah (Ta´ala) Yuko juu ya ´Arshi Yake na tunaziamini zile sifa Zake zilizopokelewa na Sunnah.”[7]

Ameipokea al-Bayhaqiy katika ”al-Asmaa’ was-Swifaat”.

Na amesema Imaam Muwafaq ad-Diyn: Imenifikia kutoka kwa Abuu Haniyfah – Allaah Amrehemu – kwamba amesema: Mtu yeyote anayekataa kuwa Allaah yuko mbinguni basi amekufuru.

Na amesema Maalik: Allaah yuko mbinguni, na elimu Yake iko kila mahali. Ameipokea…

[1] 19:52

[2] 7:143

[3] Swahiyh kwa mujibu wa adh-Dhahabiy katika “al-´Uluww”, uk. 129, cheni ya wapokezi ni Swahiyh kwa mujibu wa al-Albaaniy katika “Mukhtaswar-ul-´Uluww” (111).

[4] Swahiyh kwa mujibu wa adh-Dhahabiy katika “al-´Uluww”, uk. 128, cheni ya wapokezi ni Swahiyh kwa mujibu wa al-Albaaniy katika “Mukhtaswar-ul-´Uluww” (110).

[5] 51:22

[6] Cheni ya wapokezi iko wazi kama jua na imara zaidi kama nguzo kwa mujibu wa adh-Dhahabiy katika “al-´Uluww”, uk. 129.

[7] al-Albaaniy amesema:

”Ni Swahiyh kwa mujibu wa Ibn Taymiyyah katika ”at-Tadmuriyyah”, na Ibn-ul-Qayyim akaafikiana naye katika “Ijtimaa´-ul-Juyuush al-Islaamiyyah”, uk. 43.  Mtunzi amesema katika ufupisho wake kwamba ”Wapokezi wake ni maimamu na wenye kuaminika”.” (Mukhtaswar-ul-´Uluww (121))

  • Muhusika: Imaam Muhammad bin Ahmad bin ´Abdil-Haadiy al-Maqdisiy (afk. 744)
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Kalaam ´alaa Mas-alat-il-Istiwaa’ ´alaal-´Arsh, uk. 48-50
  • Imechapishwa: 21/12/2025