10. Hivi ndivo wanavosema wajinga juu ya mgawanyiko wa Tawhiyd

Mgawanyiko huu wa Tawhiyd katika mafungu matatu ni jambo limechukuliwa kutoka katika Qur-aan na Sunnah. Sio mgawanyiko uliozuliwa kama wanavoona wajinga na wapotevu wa leo:

يُرِيدُونَ لِيُطْفِئُوا نُورَ اللَّـهِ بِأَفْوَاهِهِمْ وَاللَّـهُ مُتِمُّ نُورِهِ وَلَوْ كَرِهَ الْكَافِرُونَ

“Wanataka kuizima nuru ya Allaah kwa midomo yao, lakini Allaah ni Mwenye kuitimiza nuru Yake japokuwa makafiri watachukia.”[1]

Mgawanyiko hautokamani na elimu ya falsafa na kanuni za watu wa mantiki wanaoongea pasi na elimu. Mgawanyiko huu umejengeka juu ya Qur-aan na Sunnah. Aayah zinazozungumzia matendo ya Allaah, majina na sifa Zake ni Tawhiyd-ur-Rubuubiyyah. Aayah zinazozungumzia kwamba ´ibaadah anafanyiwa Allaah pekee ni Tawhiyd-ul-Uluuhiyyah.

[1] 61:08

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: I´aanat-ul-Mustafiyd bi Sharh Kitaab-it-Tawhiyd, uk. 25
  • Imechapishwa: 23/07/2019