Suala la tatu ni katika mambo ambayo ni wajibu zaidi. Kila muislamu mwanaume na mwanamke anapaswa kujua kuwa haifai kwake akawa na mapenzi kwa washirikina au akawapenda. Yule anayemtii Allaah na Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na anampwekesha Allaah (Jalla wa ´Alaa) ni lazima kwake kujenga uadui na kuwachukia makafiri kwa ajili ya Allaah. Haijuzu kwake kujenga nao urafiki na kuwapenda. Allaah (Ta´ala) amesema:

لَّا تَجِدُ قَوْمًا يُؤْمِنُونَ بِاللَّـهِ وَالْيَوْمِ الْآخِرِ يُوَادُّونَ مَنْ حَادَّ اللَّـهَ وَرَسُولَهُ

“Hutokuta watu wanaomuamini Allaah na siku ya Mwisho
kuwa wanawapenda wale wanaopinzana na Allaah na Mtume Wake… “

Bi maana ee Muhammad, hakika huwezi kupata waumini wakweli wako namna hiyo. Allaah (Ta´ala) amesema:

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا تَتَّخِذُوا الْيَهُودَ وَالنَّصَارَىٰ أَوْلِيَاءَ ۘ بَعْضُهُمْ أَوْلِيَاءُ بَعْضٍ ۚ وَمَن يَتَوَلَّهُم مِّنكُمْ فَإِنَّهُ مِنْهُمْ ۗ إِنَّ اللَّـهَ لَا يَهْدِي الْقَوْمَ الظَّالِمِينَ

“Enyi mlioamini! Msiwafanye mayahudi na manaswara marafiki – wao kwa wao ni marafiki – na yeyote atakayewafanya marafiki basi yeye ni katika wao. Hakika Allaah haongoi watu madhalimu.” (05:51)

قَدْ كَانَتْ لَكُمْ أُسْوَةٌ حَسَنَةٌ فِي إِبْرَاهِيمَ وَالَّذِينَ مَعَهُ إِذْ قَالُوا لِقَوْمِهِمْ إِنَّا بُرَآءُ مِنكُمْ وَمِمَّا تَعْبُدُونَ مِن دُونِ اللَّـهِ كَفَرْنَا بِكُمْ وَبَدَا بَيْنَنَا وَبَيْنَكُمُ الْعَدَاوَةُ وَالْبَغْضَاءُ أَبَدًا حَتَّىٰ تُؤْمِنُوا بِاللَّـهِ وَحْدَهُ

“Hakika mna kigezo kizuri kwa Ibraahiym na wale walio pamoja naye, walipowaambia watu wao: “Hakika sisi tumejitenga mbali nanyi na yale mnayoyaabudu badala ya Allaah, tunakukanusheni na umedhihirika baina yetu na baina yenu uadui na bughudha milele mpaka mtapomuamini Allaah pekee.” (60:04)

Kwa hiyo ni wajibu kuwachukia na kujenga uadui dhidi ya maadui wa Allaah na kuwapenda waumini. Hivi ndivyo anavyokuwa muumini anawapenda mawalii wa Allaah na anashirikiana nao katika kheri. Sambamba na hilo anawachukia na kuwabughudhi maadui wa Allaah na kujenga uadui nao hata kama anawalingania katika Uislamu na akawaacha waishi katika nchi yake na huku anachukua kodi kutoka kwao. Kwa mfano hio ni kazi ya mtawala. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alichukua kodi kutoka kwa mayahudi, wakristo na waabudu moto ili waweze kuishi chini yake. Pamoja na hayo wanatakiwa kuchukiwa na wasipendwe. Endapo watakataa kuingia katika Uislamu na kulipa kodi wanatakiwa kupigwa vita ikiwa kuna uwezo wa kufanya hivo. Hukumu hizi zinawahusu mayahudi, wakristo na waabudu moto tu.

Kuhusu makafiri wengine waliobaki, kodi haikubaliwi kutoka kwao. Wanatakiwa kupigwa vita mpaka waingie katika Uislamu. Mfano wa watu hao ni waabudu mizimu na wakomunisti. Kama tulivyosema wanatakiwa kupigwa vita kama kuna uwezo wa kufanya hivo. Allaah (Subhaanah) amesema:

وَقَاتِلُوهُمْ حَتَّىٰ لَا تَكُونَ فِتْنَةٌ وَيَكُونَ الدِّينُ كُلُّهُ لِلَّـهِ ۚ فَإِنِ انتَهَوْا فَإِنَّ اللَّـهَ بِمَا يَعْمَلُونَ بَصِيرٌ

“Piganeni nao mpaka kusiweko fitnah na ´ibaadah zote ziwe kwa ajili ya Allaah. Na wakikoma, basi hakika Allaah anaona yale wanayoyatenda.” 08:39

انفِرُوا خِفَافًا وَثِقَالًا وَجَاهِدُوا بِأَمْوَالِكُمْ وَأَنفُسِكُمْ فِي سَبِيلِ اللَّـهِ ۚذَٰلِكُمْ خَيْرٌ لَّكُمْ إِن كُنتُمْ تَعْلَمُونَ

“Tokeni mwende vitani [sawa ikiwa mnaona] wepesi na uzito – na pambaneni katika njia ya Allaah kwa mali zenu na nafsi zenu katika njia ya Allaah; hivyo ni kheri kwenu mkiwa mnajua.” (09:41)

فَإِذَا انسَلَخَ الْأَشْهُرُ الْحُرُمُ فَاقْتُلُوا الْمُشْرِكِينَ حَيْثُ وَجَدتُّمُوهُمْ وَخُذُوهُمْ وَاحْصُرُوهُمْ وَاقْعُدُوا لَهُمْ كُلَّ مَرْصَدٍ ۚ فَإِن تَابُوا وَأَقَامُوا الصَّلَاةَ وَآتَوُا الزَّكَاةَ فَخَلُّوا سَبِيلَهُمْ ۚإِنَّ اللَّـهَ غَفُورٌ رَّحِيمٌ

“Itapomalizika miezi mitukufu basi waueni washirikina, popote muwakutapo; na wachukueni na wazungukeni na wakalieni katika kila sehemu ya uvamizi. Lakini wakitubu na [wakajionyesha] kusimamisha swalah na wakatoa zakah, basi waacheni kwa amani – hakika Allaah ni Mwingi wa kusamehe, Mwenye kurehemu.” (09:05)

Kuna Aayah nyingi zenye maana kama hii.

Allaah (Ta´ala) anaamrisha vita kama kuna uwezo wa kufanya hivo. Allaah (´Azza wa Jall) amesema vilevile:

لَا يُكَلِّفُ اللَّـهُ نَفْسًا إِلَّا وُسْعَهَا

“Allaah haikalifishi nafsi yoyote ila kwa kadiri ya uwezo wake.” (02:286)

فَاتَّقُوا اللَّـهَ مَا اسْتَطَعْتُمْ

“Basi mcheni Allaah muwezavyo.” (64:16)

Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) mwenyewe hakuwapiga vita washirikina mpaka pale alipokuwa na uwezo wa kufanya hivo. Kisha Allaah (Ta´ala) akasema:

أُولَـٰئِكَ كَتَبَ فِي قُلُوبِهِمُ الْإِيمَانَ وَأَيَّدَهُم بِرُوحٍ مِّنْهُ

“Hao [Allaah] Amewaandikia katika nyoyo zao imani na Akawatia nguvu kwa Roho kutoka Kwake.” (58:22)

Bi maana anawapa nguvu kwa nguvu kutoka Kwake.

  • Mhusika: Sharh Thalaathat-il-Usuwl, uk. 15
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Thalaathat-il-Usuwl, uk. 16-18
  • Imechapishwa: 15/10/2016