10. al-Albaaniy na harakati za kisiasa

Jambo la nane amesema kwamba al-Albaaniy ana mrengo wa kisiasa. Dogo tuwezalo kusema kwamba uongo huu ni kama ule uliotangulia. Mtu mwovu kumtuhumu mtu ambaye ameutumia umri wake mrefu akiwa katika Maktabah za kidini, baina ya vitabu vyake, akifanya utafiti na kutunga, akitunga kwa ajili ya vizazi, akiisafisha Sunnah kutokamana na visivyofaa kama vile Hadiyth zilizozuliwa na dhaifu na akajitolea muhanga starehe yake, usingizi wake, ladha ya maisha yake, wakati wake na umri wake wa miaka tisini kwa ajili ya kuutumikia Ummah wa Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kwa vitabu vitukufu kimanufaa – kumtuhumu malengo ya kisiasa kwa sababu tu alisema neno moja au mawili ambayo pia yanaweza kufahamika kwa njia nzuri si jengine isipokuwa ni dhuluma na ukandamizaji.

Mimi najitenga mbali na dhuluma na ukandamizaji huu mbele ya Allaah! Sisemi kuwa Shaykh al-Albaaniy (Rahimahu Allaah) amekingwa na kukosea katika Ijtihaad zake, ni mamoja inapokuja katika Fiqh au katika kuzigawa kwake Hadiyth. Yeye ni kama Mujtahiduun wengine wote; akipatia, basi analipwa mara mbili, na akikosea, analipwa mara moja[1]. Wakati fulani anaweza kuleta Ijtihaad za kimakosa, lakini kila mmoja yanakubaliwa maneno yake na kurudishwa isipokuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).

[1] Abu Daawuud (3574) na Ibn Maajah (2314). Swahiy kwa mujibu wa al-Albaaniy katika ”Swahiyh Sunan Ibn Maajah” (1872).

  • Mhusika: ´Allaamah Ahmad bin Yahyaa an-Najmiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Fath ar-Rabbaaniy fiyd-Difaa´ ´an-ish-Shaykh Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy, uk. 28-29
  • Imechapishwa: 16/11/2018