Kuna sampuli mbili ya tofauti zinazopingana za tafsiri ya Qur-aan. Ya kwanza inayotokana na nukuu (النقل) peke yake. Nyingine inaweza kutambulika kwa njia nyingine. Kwa sababu elimu ni ama nukuu iliyothibiti au dalili uliochanganuliwa.
Chenye kunukuliwa ima kitokane na ambaye amekingwa na makosa au kutoka kwa ambaye hakukingwa na makosa. Wakati fulani kuna uwezekano wa kujua kile kilichonukuliwa kama ni sahihi au ni dhaifu, pasi na kujali kimetokana na ambaye amekingwa na makosa au ambaye hakukingwa na makosa, na wakati mwingine haiwi hivo. Hii ni aina ya pili ya kile kinachonukuliwa, nayo ni yale ambayo hatuwezi kuthibitisha moja kwa moja juu ya usahihi wake. Mara nyingi maudhui yake hayana faida yoyote na kuzungumza juu yake hakuna umuhimu wowote. Ama yale ambayo waislamu wanayahitajia, Allaah ameijaalia haki katika jambo hilo kwa dalili.
Mfano wa yale mambo yasiyo na faida na wala hakuna dalili juu ya usahihi wake ni kutofautiana kwao juu ya rangi ya mbwa wa watu wa Pango, ni kiungo gani ambacho Muusa alimpiga yule ng´ombe wa wana wa israaiyl, ukubwa wa safina ya Nuuh na aina ya mbao yake, jina la yule kijana ambaye aliuliwa na al-Khadhwir na kadhalika. Njia pekee ya kuyajua mambo hayo ni kupitia wahy tu. Ikiwa jambo limehifadhiwa kwa usahihi kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam), kwa mfano jina la rafiki yake Nabii Muusa kwamba ni al-Khadhwir, basi hili ni jambo lililothibitishwa. Lakini yale yasiyokuwa hivyo, bali yamechukuliwa kutoka kwa watu wa Kitabu, kama yale yaliyopokelewa kutoka kwa K’ab, Wahb, Muhammad bin Ishaaq na wengine waliopokea kutoka kwa watu wa Kitabu, haya hayapaswi kuthibitishwa kuwa ya kweli au kukataliwa kuwa si ya kweli isipokuwa kwa hoja. Imethibiti ya kwamba Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) amesema:
“Mnaposimuliwa na watu wa Kitabu, basi msiwasadikishe wala msiwakadhibishe. Inawezekana wakakusimulieni ya haki na hivyo mkawakadhibisha au wakakusimulieni kwa batili na hivyo mkawasadikisha.”[1]
[1] Ahmad (4/136), Abu Daawuud (3644) na Ibn Hibbaan (110). Dhaifu kwa mujibu wa al-Albaaniy katika “Dhwa´iyf Sunan Abiy Daawuud” (3644).
- Muhusika: Shaykh-ul-Islaam Ahmad bin Taymiyyah
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Muqaddimah fiy Usuwl-it-Tafsiyr, uk. 48-50
- Imechapishwa: 31/03/2025
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window) Telegram
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window) WhatsApp
- Click to print (Opens in new window) Print
- Click to email a link to a friend (Opens in new window) Email
- Click to share on Facebook (Opens in new window) Facebook
- Click to share on X (Opens in new window) X
- Click to share on Pocket (Opens in new window) Pocket