29 – Abul-Husayn Ahmad bin al-Husayn bin Ahmad al-Waa-idhw ametukhabarisha: Nimemsikia Abu ´Abdillaah ar-Ruudhbaariy akisema:

”Anayetoka kuiendea elimu kwa ajili ya elimu, elimu haitomfaa kitu. Na anayetoka kuiendea elimu kwa ajili kuifanyia kazi elimu kimatendo, elimu itamfaa ijapo elimu yake itakuwa ndogo.”

30 – Amesema: Nimemsikia Abu ´Abdillaah ar-Ruudhbaariy akisema:

”Elimu inategemea matendo. Matendo yanategemea kumtakasia nia Allaah. Kumtakasia nia Allaah kunapelekea uelewa kutoka kwa Allaah (´Azza wa Jall).”

31 – al-Hasan bin Abiy Bakr bin Shaadhaan ametukhabarisha: Abul-Hasan ´Aliy bin Muhammad bin az-Zubayr al-Kuufiy ametukhabarisha: al-Hasan bin ´Aliy bin ´Affaan ametuhadithia: Zayd bin al-Hubaab ametuhadithia, kutoka kwa Hafsw bin Sulaymaan, kutoka kwa Ibn Shaadhaan, ambaye pengine anaitwa Ja´far bin Sulaymaan, ambaye ameeleza kuwa amemsikia Maalik bin Diynaar akisema:

”Mja akitafuta elimu kwa ajili kufanya matendo, elimu yake humtiisha. Na akiitafuta kwa ajili ya kitu kingine, basi hamzidishii jengine isipokuwa tu kuwa mtenda dhambi na mwenye kiburi.”

32 – Abu ´Abdillaah Muhammad bin ´Abdil-Waahid bin Muhammad bin Ja´far ametukhabarisha: ´Abdul-´Aziyz bin Ja´far al-Khiraqiy ametuhadithia: ´Ubaydullaah bin A´yan ametuhadithia: Ishaaq bin Abiy Israa-iyl ametuhadithia: Ja´far bin Sulaymaan ametuhadithia: Nimemsikia Maalik bin Diynaar akisema:

”Mwenye kutafuta elimu kwa ajili ya kufanya matendo, elimu yake humtiisha. Na mwenye kuitafuta kwa lengo jengine lisilokuwa kufanya matendo, humzidishia tu kiburi.”

33 – Muhammad bin Ahmad bin Rizq ametukhabarisha: Ja´far bin Muhammad bin Nuswayr al-Khuldiy ametukhabarisha: Muhammad bin ´Abdillaah bin Sulaymaan al-Hadhwramiy ametuhadithia: Sa´iyd bin ´Amr  ametuhadithia: Ja´far bin Sulaymaan ametuhadithia: Maalik bin Diynaar amesema:

”Mja akitafuta elimu kwa ajili ya matendo, elimu yake humtiisha. Na akiitafuta kwa lengo jengine lisilokuwa kufanya matendo, humzidishia tu kiburi.”

34 – Abul-Qaasim ´Abdur-Rahmaan bin Muhammad bin ´Abdillaah as-Sarraaj ametukhabarisha huko Naysaabuur: Abul-Hasan Ahmad bin Muhammad bin ´Abduus at-Twaraa-ifiy ametukhabarisha: ´Uthmaan bin Sa´iyd ad-Daarimiy ametuhadthia: Zakariyyaa bin Naafiy´ al-Filastwiyniy ametuhadthia: ´Abbaad bin ´Abbaad (al-Khawwaas) ar-Ramliy ametuhadthia, kutoka kwa Ibn Shawdhab, kutoka kwa Matwar, aliyesema:

”Elimu bora ni ile yenye kunufaisha. Hakika mambo yalivyo ni kwamba Allaah hunufaisha kwa elimu kwa yule mwenye kujifunza kisha baada ya hapo akaitendea kazi. Haimnufaishi kitu yule mwenye kuijua kisha akaiacha.”

35 – Abu Muhammad al-Hasan bi ´Aliy bin Muhammad al-Jawhariy ametukhabarisha: Abu ´Umar Muhammad bin al-´Abbaas al-Khazzaaz ametuhadithia: Yahyaa bin Muhammad bin Swaa´id ametukhabarisha: al-Husayn bin al-Hasan al-Marwaziy ametuhadithia: Ibn-ul-Mubaarak ametukhabarisha: Hariyz bin ´Uthmaan ametukhabarisha, kutoka kwa Habiyb bin ´Ubayd ar-Rahabiy, ambaye amesema:

”Jifunzeni elimu, muielewe na mnufaike nayo. Msijifunze nayo kwa ajili tu ya kujipamba nayo. Hakika mkiishi maisha marefu mtakuja kuwaona watu ambao wanajipamba kwa elimu kama ambavo mtu anajipamba kwa nguo yake.”

  • Mhusika: Imaam Abu Bakr Ahmad bin ´Aliy al-Khatwiyb al-Baghdaadiy (afk. 463)
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Iqtidhwaa’-ul-´Ilm al-´Amal, uk. 31-34
  • Imechapishwa: 08/05/2024
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy