09. Tusemeje sisi ikiwa Maswahabah walikuwa hawajiaminishi nafsi zao?

Ibn Abiy Mulaykah (Rahimahu Allaah) amesema:

“Nimekutana na Maswahabah wa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) thelathini. Hakuna yeyote katika wao ambaye alisema kuwa yeye yuko juu ya imani ya Jibriyl na Mikaaiyl. Wote walikuwa wanachelea unafiki juu ya nafsi zao.”

Huyu ni Taabi´iy mtukufu. Wote walikuwa wanaogopa na wote walikuwa wakishika tahadhari. Baadhi yao wamesema:

“Ni nani atakayejiaminisha na mtihani baada ya Ibraahiym ambaye alisema:

وَاجْنُبْنِي وَبَنِيَّ أَن نَّعْبُدَ الْأَصْنَامَ  رَبِّ إِنَّهُنَّ أَضْلَلْنَ كَثِيرًا مِّنَ النَّاسِ

“Unikinge mimi na wanangu kuabudu masanamu.” Ee Mola wangu! Hakika hao wamepoteza wengi kati ya watu.”[1]

Anaogopa asije kupatwa na yale yaliyowapata wengi. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa akimlilia Mola Wake na akimuomba (Subhaanahu wa Ta´ala) akisema:

اللهم اغفر لي ذنبي كله، دقه وجله

“Ee Allaah! Nisamehe dhambi zangu zote nyeti na za dhahiri.”[2]

Siku zote alikuwa (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akimuomba Mola Wake kwa kusema:

اللهم اغفر لي خطيئتي وجهلي، وإسرافي في أمري، وما أنت أعلم به مني

“Ee Allaah! Nisamehe makosa yangu, ujinga wangu, kupindukia kwangu katika amri yangu na yale ambayo Wewe ni mjuzi zaidi kuliko mimi.”[3]

اللهم يا مقلب القلوب ثبت قلبي على دينك

“Ee Allaah! Ee Mwenye kuzipindukia nyoyo! Uthibitishe moyo wangu katika dini Yako.”[4]

Anasema hivi ilihali yeye ndiye Nabii na Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Kiumbe mbora (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Aliwahi kusema:

“Ninaapa kwa Allaah, si vyenginevyo, ya kwamba mimi ndiye mwenye kumuogopa na kumcha Allaah zaidi yenu.”[5]

Ameapa kwa jina la Allaah kwamba yeye ndiye mtu anayemcha Allaah zaidi na mtu ambaye anamuogopa Allaah zaidi. Haya ni kutokana na imani na uchaji Wake mkubwa:

“Ninaapa kwa Yule ambaye nafsi yangu iko mikononi Mwake. Hakika mimi ndiye mwenye kumuogopa na kumcha Allaah zaidi yenu.”

[1] 16:35-36

[2]Muslim (483).

[3] al-Bukhaariy (6398) na Muslim (2729).

[4] at-Tirmidhiy (2140).

[5] al-Bukhaariy (5063) na Muslim (1401).

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Kashf-ish-Shubuhaat, uk. 25-26
  • Imechapishwa: 13/10/2021