Swali: Je, inafaa kwa mfungaji kutumia dawa ya meno ilihali amefunga mchana wa Ramadhaan?

Jibu: Hapana neno kufanya hivo pamoja na kuchunga asimeze kitu. Kama ambavo imewekwa katika Shari´ah mfungaji kutumia Siwaak mwanzoni mwa mchana na mwishoni mwake. Baadhi ya wanachuoni wameeonelea inachukiza kwa mfungaji kutumia Siwaak baada ya jua kupinduka. Lakini hata hivyo ni maoni yasiyokuwa na nguvu. Maoni ya sawa ni kwamba haikuchukizwa. Hayo ni kutokana na kuenea kwa maneno ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

Siwaak ni yenye kusafisha mdomo na ni yenye kumridhisha Mola.”

Ameipokea an-Nasaa´iy kwa cheni ya wapokezi Swahiyh kutoka kwa ´Aaishah (Radhiya Allaahu ´anhaa).

Vilevile amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Lau nisingeliutia uzito Ummah wangu, basi ningeliwaamrisha watumie Siwaak katika kila swalah.”

Ameipokea al-Bukhaariy na Muslim.

Hapa kunaingia swalah ya Dhuhr na ´Aswr, jambo ambalo ni baada ya jua kupondoka.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ashyaa´ laa tufsid-is-Swawm, uk. 09-10
  • Imechapishwa: 31/03/2021