Abu Ja´far at-Twahaawiy (Rahimahu Allaah) amesema:
34 – Yeye ndiye mwisho wa Manabii, kiongozi wa wenye kumcha Allaah, bwana wa Mitume na kipenzi wa Mola wa walimwengu.
MAELEZO
´Aqiydah hii imethibiti katika Hadiyth nyingi na zinazotambulika vyema ambazo ummah wamezipokea kwa kuzikubali. Katika maelezo ya Ibn Abiyl-´Izz ametaja baadhi yazo, kwa sababu hiyo zinafidisha elimu na yakini.
Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ndiye bwana wa Mitume kwa yakini kabisa. Miongoni mwa masikitiko makubwa ni kuwa ´Aqiydah hii hawaiamini wale wanaoshurutisha kwamba Hadiyth ni lazima ipokelewe na wapokezi wengi. Ni vipi basi wataiamini, kukiwemo Shaykh Shaltuut na wengineo, waliosema wazi kuwa ´Aqiydah ni lazima ichukuliwe kutoka ndani ya Qur-aan peke yake? Nimewaraddi wote hawa kwa njia ishirini katika kitabu changu ”Wujuwb-ul-Akhdh bi Hadiyth-il-Aahaad”. Mwishoni mwa kitabu hicho nimetaja Hadiyth ishirini na zilizothibiti ambazo zinawalazimu watu hawa kuzikanusha na kutoziamini kwa sababu ya fikira yao. ´Aqiydah hii ni moja katika hizo.
Mtunzi wa kitabu (Rahimahu Allaah) amesema:
”… na kipenzi (حبيب) wa Mola wa walimwengu.”
Bali ni kipenzi wa hali ya juu (خليل) wa Mola wa walimwengu. Mapenzi ya hali ya juu ndio yenye ngazi ya juu zaidi na kamilifu zaidi kuliko mapenzi ya kawaida. Kwa ajili hiyo Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Hakika Allaah amenifanya kuwa kipenzi Wake wa hali ya juu kama alivyomfanya Ibraahiym kuwa kipenzi Wake wa hali ya juu.”[1]
Kwa ajili haikuthibiti katika Hadiyth yoyote kwamba yeye (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ni kipenzi (حبيب) wa Allaah.
[1] Muslim (532).
- Muhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: al-´Aqiydah at-Twahaawiyyah – Sharh wa Ta´liyq, uk. 19-21
- Imechapishwa: 15/09/2024
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)