Kama amelazimika kuunganisha basi aunganishe mpaka wakati wa mwisho wa usiku. Kwa msemo mwingine afunge mchana na sehemu kubwa ya usiku kisha afanye chakula chake cha daku kuanzia daku mpaka daku nyingine. Hapana vibaya kufanya hivo. Lakini kule kukata kwake swawm mwanzoni mwa usiku ndio bora zaidi. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Watu hawatoacha kuwa katika kheri muda wa kuwa wanaharakisha kukata swawm.”[1]

Allaah (Subhaanah) amesema:

“Waja wanaopendeza zaidi kwangu ni wale wanaoharakisha kukata swawm.”[2]

Kwa hivyo Sunnah ni kwa mfungaji ni yeye aharakishe kukata swawm punde tu jua likishazama. Lakini akiunganisha mpaka wakati wa daku na akaacha kula na kunywa mpaka wakati wa daku hapana neno kutokana na Hadiyth hii ya Abu Sa´iyd na nyenginezo zilizokuja zikiwa na maana kama hii. Lakini imechukizwa kwake kuunganisha usiku na mchana na ni jambo lisilotakikana. Sio haramu. Lakini imechukizwa. Kwa ajili hii imekuja katika Hadiyth ya Abu Hurayrah:

“Akaunganisha nao siku moja, kisha siku nyingine kisha akaona mwezi mwandamo ambapo akasema: “Nisingeona mwezi basi ningekuzidishieni… “

Kana kwamba anawakemea pale walipokataa kuacha jambo hilo. Hii inafahamisha kuwa kuunganisha ni sahihi na ni kitu kinachofaa. Lakini imechukizwa na kukatazwa. Sio haramu. Kwa sababu yeye aliunganisha nao. Ingelikuwa ni haramu basi asingeunganisha nao na wala asingewafanya kuingia ndani ya dhambi. Lakini inajulisha kuwa imechukizwa kwa ajili ya kuwafanyia upole na kuwaonea huruma. Kwa hiyo haitakikani kwao kuunganisha. Imechukizwa kwao kuunganisha kutokana na Hadiyth hii Swahiyh ambayo inakataza na kukemea jambo hilo. Amefanya hivo kwa sababu ya kuwahurumia waja, kuwafanyia wema, kuwafanyia upole na kuwafanyia kutoka kwa Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala).

[1] Ahmad (21312). Ameipa nguvu al-Albaaniy katika ”as-Swahiyhah” (1773).

[2] Ahmad (7241), at-Tirmidhiy (700) na Ibn Khuzaymah (2062). Ameisahihisha Ibn Hibbaan (04/558), al-Bayhaqiy (04/237). Ni dhaifu kwa mujibu wa al-Albaaniy katika “Dhwa´iyf Sunan-it-Tirmidhiy” (01/80) na katika “Dhwa´yf-ut-Targhiyb wat-Tarhiyb (01/163)).

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Ifhaam fiy Sharh ´Umdat-il-Ahkaam (01/415-417)
  • Imechapishwa: 24/03/2022