09. Muhammad alitumwa kwa watu wanaomwamini Allaah

Shaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (Rahimahu Allaah) amesema:

Allaah alimtuma kwa watu ambao wanaabudu, wanahiji, wanatoa swadaqah na wanamdhukuru Allaah kwa wingi.

MAELEZO

Allaah alimtuma Mtume Wake Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kwa watu wenye kufanya ´ibaadah. Lakini ´ibaadah zao zilikuwa za batili na zisizokuwa na dalili yoyote. Walikuwa wakitoa swadaqah na wakifanya matendo mengi ya kheri. Lakini hayakuwafaa kitu kwa sababu walikuwa ni makafiri. Miongoni mwa masharti ya kujikurubisha kwa Allaah (Ta´ala) ni mtu awe muislamu, jambo ambalo watu hawa hawakuwa nalo.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Kashf-ish-Shubuhaat, uk. 20
  • Imechapishwa: 04/10/2023