3 – Katika kusherehekea maulidi kuna kuhuisha ukumbusho wa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Tunajibu hilo kwa kusema ya kwamba kuhuisha kumkumbuka Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ni kitu anachokifanya muislamu na amefungamana nacho kila kunapotajwa jina lake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) katika adhaana, Iqaamah, Khutbah, anapotamka shahaadah mbili baada ya kutawadha, anapomswalia Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) katika Tashahhud, kila kunapotajwa jina lake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na kila pale ambapo muislamu anafanya tendo jema – ni mamoja ikiwa ni cha wajibu au kilichopendekezwa miongoni mwa yale yaliyoweka Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) katika Shari´ah – kwa kufanya hivo anakuwa ni mwenye kumkumbuka na anaandikiwa ujira sawa na ujira wa mtendaji. Namna hii umri wote wa muislamu anakuwa ni mwenye kuhuisha ukumbusho wa Mtume katika yale aliyoweka Allaah katika Shari´ah na anakuwa ni mwenye kufungamana naye usiku na mchana. Na si kumkumbuka wakati wa kuzaliwa tu, jambo ambalo ni Bid´ah na ni kwenda kinyume na Sunnah zake. Hakika kusherehekea maulidi ni kitu kinachomtenga na kumuweka mtu mbali na Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ni mwenye kujitosheleza na sherehe hii ya kizushi kwa yale aliyomuwekea Allaah katika Shari´ah pale alipomuadhimisha na kumheshimisha. Allaah (Ta´ala) amesema:
وَرَفَعْنَا لَكَ ذِكْرَكَ
“Tukanyanyulia juu utajo wako.”[1]?
Allaah anapotajwa katika adhaana, Iqaamah na Khutbah basi kunaambatanishwa pia jina la Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Hilo limetosheleza kuwa ni maadhimisho, mapenzi na kumbukumbu kwa yule anayetaka kumkumbuka Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).
Allaah (Subaahahu wa Ta´ala) hakukipa umuhimu kuzaliwa kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Alichotilia umuhimu ni kule kutumilizwa kwake pale aliposema:
لَقَدْ مَنَّ اللَّـهُ عَلَى الْمُؤْمِنِينَ إِذْ بَعَثَ فِيهِمْ رَسُولًا مِّنْ أَنفُسِهِمْ
”Hakika Allaah amewaneemesha waumini pale alipomtuma kwao Mtume anayetokana na wao wenyewe.”[2]
هُوَ الَّذِي بَعَثَ فِي الْأُمِّيِّينَ رَسُولًا مِّنْهُمْ
“Yeye ndiye aliyempeleka Mtume kwa wasiojua kusoma wala kuandika anayetokamana na wao.”[3]
[1] 94:04
[2] 03:164
[3] 62:2
- Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Huquwq-un-Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) bayn al-Ijlaal wal-Ikhlaal, uk. 152-153
- Imechapishwa: 06/09/2025

Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Huquwq-un-Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) bayn al-Ijlaal wal-Ikhlaal, uk. 152-153
Imechapishwa: 06/09/2025
https://firqatunnajia.com/09-maulidi-ni-ukumbusho-wa-mtume/