Huyu hapa Muusa (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ambaye alitishiwa na Fir´awn kuuliwa:

ذَرُونِي أَقْتُلْ مُوسَىٰ وَلْيَدْعُ رَبَّهُ ۖ إِنِّي أَخَافُ أَن يُبَدِّلَ دِينَكُمْ أَوْ أَن يُظْهِرَ فِي الْأَرْضِ الْفَسَادَ

“Niacheni nimuue Muusa, naye amwite Mola wake! Hakika mimi nachelea asije kukubadilishieni dini yenu au adhihirishe uharibifu katika ardhi.”[1]

Kwa hivyo akatishiwa kuuliwa. Lakini mwisho mwema ulikuwa kwa Muusa (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

فَوَقَاهُ اللَّـهُ سَيِّئَاتِ مَا مَكَرُوا ۖ وَحَاقَ بِآلِ فِرْعَوْنَ سُوءُ الْعَذَابِ

“Basi Allaah akamkinga na maovu ya yale waliyoyapangia njama na watu wa Fir’awn ikawazunguka adhabu mbaya kabisa.”[2]

Huyu hapa ´Iysaa (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ambaye alipatwa na maudhi chungumzima mpaka mayahudi wakamrushia tuhuma kwamba ni mtoto wa uzinzi na wakamuua na wakamsulubu kwa mujibu wa madai yao. Lakini Allaah amesema:

وَمَا قَتَلُوهُ وَمَا صَلَبُوهُ وَلَـٰكِن شُبِّهَ لَهُمْ ۚ وَإِنَّ الَّذِينَ اخْتَلَفُوا فِيهِ لَفِي شَكٍّ مِّنْهُ ۚ مَا لَهُم بِهِ مِنْ عِلْمٍ إِلَّا اتِّبَاعَ الظَّنِّ ۚ وَمَا قَتَلُوهُ يَقِينًا بَل رَّفَعَهُ اللَّـهُ إِلَيْهِ ۚ وَكَانَ اللَّـهُ عَزِيزًا حَكِيمًا

“Wala hawakumuua wala hawakumsulubu lakini walishabihishiwa tu. Hakika wale waliotofautiana juu yake wamo katika shaka kutokamana nalo – hawana ujuzi nalo kabisa isipokuwa kufuata dhana tu. Kwa yakini hawakumuua. Bali Allaah alimnyanyua Kwake. Allaah daima ni Mwenye nguvu zisizoshindika, Mwenye hekima.”[3]

Akaokolewa kutokamana nao.

[1] 40:26

[2] 40:45

[3] 04:157-158

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Zaad Daa´iyah ila Allaah, uk. 15-16
  • Imechapishwa: 02/11/2021