Huyu hapa Ibraahiym (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ambaye alikataliwa na watu wake bali wakafikia mpaka kumchafua kati ya watu:

قَالُوا فَأْتُوا بِهِ عَلَىٰ أَعْيُنِ النَّاسِ لَعَلَّهُمْ يَشْهَدُونَ

“Wakasema: “Mleteni mbele ya macho ya watu ili wapate kushuhudia.””[1]

Kisha wakamtishia kumchoma moto:

قَالُوا حَرِّقُوهُ وَانصُرُوا آلِهَتَكُمْ إِن كُنتُمْ فَاعِلِينَ

“Wakasema: “Mchomeni moto na mnusuru waungu wenu, mkiwa ni wafanyao nusura.””[2]

Wakawasha moto mkubwa na wakamrusha kwa manati kubwa kutokana na kuwa kwao mbali nao kwa sababu ya ukali wake. Lakini Allaah akasema:

قُلْنَا يَا نَارُ كُونِي بَرْدًا وَسَلَامًا عَلَىٰ إِبْرَاهِيمَ

“Tukasema: “Ee moto! Kuwa baridi na salama kwa Ibraahiym!”[3]

Moto ukawa ni wenye baridi iliosalama na akaokoka nao. Hivyo mwisho mwema ukawa kwa Ibraahiym:

وَأَرَادُوا بِهِ كَيْدًا فَجَعَلْنَاهُمُ الْأَخْسَرِينَ

“Wakamkusudia njama, lakini Tukawafanya wao ndio wenye kukhasirika.”[4]

[1] 21:61

[2] 21:68

[3] 21:69

[4] 21:70

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Zaad Daa´iyah ila Allaah, uk. 15
  • Imechapishwa: 02/11/2021