09. Maamrisho ya Ahmad ya kushikamana na Sunnah

4- Ahmad bin Hanbal (Rahimahu Allaah)

Imaam Ahmad ni mmoja katika maimamu ambao wamekusanya Sunnah kiasi kikubwa, wameshikamana nayo barabara. Kiasi cha kwamba alikuwa akichukia kuandikwa kwa vitabu kuhusu mambo ya mataga na maoni[1]. Kwa ajili hiyo amesema:

1- “Msinifuate mimi kichwa mchunga. Msimfuate Maalik, wala ash-Shaafi´iy, wala al-Awzaa´iy wala ath-Thawriy. Chote kule wanakochota.”[2]

Katika upokezi mwingine imekuja:

“Usimfuate kichwa mchunga yeyote katika dini yako. Chukua yale yenye kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na Maswahabah zake. Inapokuja kwa wale Taabi´uun basi mtu ana khiyari.”

Siku nyingine alisema:

“Kufuata ina maana kwamba mtu akafuata yale yenye kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na Maswahabah zake. Inapokuja kwa Taabi´uun mtu ana khiyari.”[3]

2- ”Maoni ya al-Awzaa´iy, maoni ya Maalik na maoni ya Abu Haniyfah hayo ni maoni tu. Yote haya kwangu nayaona ni sawasawa. Hoja iko katika mapokezi.”[4]

3- “Mwenye kurudisha Hadiyth ya Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) basi yuko katika ukingo wa maangamivu.”[5]

[1] al-Manaaqib, uk. 192, cha Ibn-ul-Jawziy.

[2] al-Fulaaniy (113) na Ibn-ul-Qayyim katika ”I´laam-ul-Muwaqqi´iyn” (2/302).

[3] Abu Daawuud katika ”Masaa-il-ul-Imaam Ahmad”, uk. 276-277

[4] Ibn ´Abdil-Barr katika ”al-Jaamiy´” (2/149).

[5] al-Manaaqib, uk. 182, cha Ibn-ul-Jawziy.

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Swifatu Swalaat-in-Nabiy, uk. 47-48
  • Imechapishwa: 17/01/2019