Swali 9: Je, kuna ubaya wowote kutahadharisha mapote haya yanayoenda kinyume na mfumo wa Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah?
Jibu: Sisi tunatahadharisha kila yule mwenye kwenda kinyume kwa jumla[1] na tunasema kuwa tunashikamana na mfumo wa Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah na kuacha kila chenye kwenda kinyume na Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah. Hatujali ni mamoja uhalifu ikiwa ni mkubwa au mdogo. Kwa sababu tukichukulia wepesi wa uhalifu kuna khatari ukawa mkubwa. Uhalifu haujuzu kwa hali yoyote ile. Lililo la wajibu ni kufuata mfumo wa Ahl-us-Sunnah katika mamdo makubwa na madogo.
[1] Namna hii ndivyo walivokuwa Salaf. Hawakuwa wakinyamaza. Bali waliwakemea wale wenye kunyamaza. Muhammad bin Bandaar al-Jurjaaniy alimwambia Imaam Ahmad: “Mimi naona ugumu kusema fulani yuko kadhaa na kadhaa.” Ndipo Ahmad akasema: “Ukinyamaza wewe na mimi nikanyamaza – ni lini mjinga atajua lililo salama na lililo na ugonjwa?” (Tazama ” ”Majmuu´-ul-Fataawaa” (28/231) na ”Sharh ´Ilal at-Tirmidhiy” (1/350).)
Wakati Imaam Ahmad alipoulizwa kuhusu Husayn al-Karaabiysiy alisema:
“Ni mzushi.”
Amesema sehemu nyingine:
“Ninakutahadharisha na Husayn al-Karaabiysiy! Usizungumze naye! Usizungumze na yule anayezungumza naye!”
Alisema hivo mara nne au tano. (Tazama “Taariykh Baghdaad” (08/65).)
Salaf walikuwa wanaona kuwatahadharisha Ahl-ul-Bid´ah ni bora kuliko kufunga, kuswali na kukaa I´tikaaf. Imaam Ahmad aliulizwa linalopendeza zaidi kwake ni mtu afunge, aswali, akae I´tikaaf au atahadharishe Ahl-ul-Bid´ah. Akasema:
“Akifunga, akiswali na kufanya I´tikaaf ni jambo lenye manufaa kwake tu. Lakini akitahadharisha Ahl-ul-Bid´ah ni jambo lenye manufaa kwa waislamu.” (Tazama ”Majmuu´-ul-Fataawaa” (28/231).)
- Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
- Mfasiri: Firqatunnajia.com
- Marejeo: al-Ajwibah al-Mufiydah ´an As-ilat-il-Manaahij al-Jadiydah, uk. 30-31
- Imechapishwa: 18/02/2017
Swali 9: Je, kuna ubaya wowote kutahadharisha mapote haya yanayoenda kinyume na mfumo wa Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah?
Jibu: Sisi tunatahadharisha kila yule mwenye kwenda kinyume kwa jumla[1] na tunasema kuwa tunashikamana na mfumo wa Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah na kuacha kila chenye kwenda kinyume na Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah. Hatujali ni mamoja uhalifu ikiwa ni mkubwa au mdogo. Kwa sababu tukichukulia wepesi wa uhalifu kuna khatari ukawa mkubwa. Uhalifu haujuzu kwa hali yoyote ile. Lililo la wajibu ni kufuata mfumo wa Ahl-us-Sunnah katika mamdo makubwa na madogo.
[1] Namna hii ndivyo walivokuwa Salaf. Hawakuwa wakinyamaza. Bali waliwakemea wale wenye kunyamaza. Muhammad bin Bandaar al-Jurjaaniy alimwambia Imaam Ahmad: “Mimi naona ugumu kusema fulani yuko kadhaa na kadhaa.” Ndipo Ahmad akasema: “Ukinyamaza wewe na mimi nikanyamaza – ni lini mjinga atajua lililo salama na lililo na ugonjwa?” (Tazama ” ”Majmuu´-ul-Fataawaa” (28/231) na ”Sharh ´Ilal at-Tirmidhiy” (1/350).)
Wakati Imaam Ahmad alipoulizwa kuhusu Husayn al-Karaabiysiy alisema:
“Ni mzushi.”
Amesema sehemu nyingine:
“Ninakutahadharisha na Husayn al-Karaabiysiy! Usizungumze naye! Usizungumze na yule anayezungumza naye!”
Alisema hivo mara nne au tano. (Tazama “Taariykh Baghdaad” (08/65).)
Salaf walikuwa wanaona kuwatahadharisha Ahl-ul-Bid´ah ni bora kuliko kufunga, kuswali na kukaa I´tikaaf. Imaam Ahmad aliulizwa linalopendeza zaidi kwake ni mtu afunge, aswali, akae I´tikaaf au atahadharishe Ahl-ul-Bid´ah. Akasema:
“Akifunga, akiswali na kufanya I´tikaaf ni jambo lenye manufaa kwake tu. Lakini akitahadharisha Ahl-ul-Bid´ah ni jambo lenye manufaa kwa waislamu.” (Tazama ”Majmuu´-ul-Fataawaa” (28/231).)
Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
Mfasiri: Firqatunnajia.com
Marejeo: al-Ajwibah al-Mufiydah ´an As-ilat-il-Manaahij al-Jadiydah, uk. 30-31
Imechapishwa: 18/02/2017
https://firqatunnajia.com/09-kutahadharisha-ahl-ul-bidah/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)