Shaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (Rahimahu Allaah) amesema:

Dalili ya Malaika ni maneno Yake (Ta´ala):

وَلَا يَأْمُرَكُمْ أَن تَتَّخِذُوا الْمَلَائِكَةَ وَالنَّبِيِّينَ أَرْبَابًا

“Na wala hakuamuruni kuwafanya Malaika na Manabii kuwafanya miungu.” (03:80)

Dalili ya Mitume ni maneno Yake (Ta´ala):

وَإِذْ قَالَ اللَّـهُ يَا عِيسَى ابْنَ مَرْيَمَ أَأَنتَ قُلْتَ لِلنَّاسِ اتَّخِذُونِي وَأُمِّيَ إِلَـٰهَيْنِ مِن دُونِ اللَّـهِ ۖ قَالَ سُبْحَانَكَ مَا يَكُونُ لِي أَنْ أَقُولَ مَا لَيْسَ لِي بِحَقٍّ ۚ إِن كُنتُ قُلْتُهُ فَقَدْ عَلِمْتَهُ ۚ تَعْلَمُ مَا فِي نَفْسِي وَلَا أَعْلَمُ مَا فِي نَفْسِكَ ۚ إِنَّكَ أَنتَ عَلَّامُ الْغُيُوبِ

“Na pale Allaah atakaposema: “Ee ‘Iysaa mwana wa Maryam! Je, wewe uliwaambia watu: “Nifanyeni mimi na mama yangu kuwa ni miungu miwili pasi na ya Allaah?” Atasema: “Utakasifu ni Wako! Hainipasi mimi kusema yasiyo kuwa haki kwangu; ikiwa nimesema hayo basi kwa hakika Ungeliyajua – Unayajua yale yote yaliyomo katika nafsi yangu na wala [mimi] sijui yale yaliyomo katika Nafsi Yako. Hakika Wewe ni Mjuzi zaidi wa yaliyofichikana.” (05:116)

MAELEZO

Maneno mtunzi:

Dalili ya Malaika ni maneno Yake (Ta´ala):

وَلَا يَأْمُرَكُمْ أَن تَتَّخِذُوا الْمَلَائِكَةَ

“Na wala hakuamuruni kuwafanya Malaika… “

ni dalili yenye kufahamisha kuwa kuna ambao wanaabudu Malaika na Mitume na kwamba hii ni shirki. Waabudia makaburi hii leo wanasema:

“Ambaye anawaabudu Malaika, Mitume na watu wema sio kafiri.”

Maneno yake mtunzi:

“Dalili ya Mitume… “

hapa kuna dalili kwamba ´ibaadah wanayofanyiwa Mitume ni shirki kama ´ibaadah wanayofanyiwa masanamu. Hapa kuna Radd kwa waabudia makaburi ambao wanatofautisha kati ya hayo mawili na kusema:

“Shirki ni kuabudu masanamu.”

Hawalinganishi yule anayeabudu masanamu na ambaye anayemwabudu mawalii na watu wema. Wanapinga kumlinganisha huyu na wanadai kuwa shirki ni kule kuyaabudu masanamu peke yake. Hili ni kosa la wazi kabisa kwa njia mbili:

1 – Allaah (Jalla wa ´Alaa) amewakaripia wote katika Qur-aan na akaamrisha wapigwe vita.

2 – Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) hakutofautisha kati ya wale wenye kuabudia masanamu, Malaika na waja wema.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh al-Qawaa´id al-Arba´ah, uk. 25-26
  • Imechapishwa: 18/08/2022