71 – Duhaym ametukhabarisha: al-Waliyd bin Muslim ametukhabarisha, kutoka kwa al-Awzaa´iy, kutoka kwa az-Zuhriy, kutoka kwa Abu Salamah, kutoka kwa Abu Hurayrah, ambaye amesimulia kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Hazini mwenye kuzini pale anapozini hali ya kuwa ni muumini, na wala haibi mwenye kuiba pale anapoiba hali ya kuwa ni muumini.”[1]
al-Awzaa’iy akasema:
“Nilimuuliza az-Zuhriy: “Ee Abu Bakr, ni Hadiyth gani hiyo?” Akasema: “Ujumbe ni wenye kutoka kwa Allaah, ni jukumu la Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) kufikisha na ni juu yetu kujisalimisha.”
72 – Abu Bakr ametukhabarisha: Abu Usaamah ametukhabarisha: al-´Alaa’ bin ´Abdir-Rahmaan ametukhabarisha:
“Bedui mmoja alitujia na kusema: “Nilihamia Kuufah na nikakutana na Suwayd bin Ghaflah, ambaye alisema: “Natamani ningelikuwa na mwanamke mzuri, kitu cha kuweza kunifanya kuweza kuishi na makazi hapa kandoni kidogo.”
73 – Ibn Abiy ´Umar ametukhabarisha: Sufyaan ametukhabarisha:
“Raqabah aliulizwa kuhusu jambo na akasema: ”Mpaka kupambazuke alfajiri.” Ibn-ul-Mas’uudiy akasema: “Unasemaje ikiwa alfajiri haikupambazuka mpaka nusu ya usiku?” Akasema: ”Lazimiana na kunyamaza, ee mpwa wangu!”
74 – Abu Bakr ametukhabarisha: ´Aliy bin Hafsw ametukhabarisha: Shu´bah ametukhabarisha, kutoka kwa Khubayb bin ´Abdir-Rahmaan, kutoka wa Hafsw bin ´Aaswim, kutoka kwa Abu Hurayrah, ambaye ameeleza Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Inatosha kwa mtu kuwa ni dhambi kuzungumzia kila anachokisikia.”[2]
75 – Abu Bakr ametukhabarisha: Ibn Mahdiy ametukhabarisha, kutoka kwa Sufyaan, kutoka kwa Abu Ishaaq, kutoka kwa Abul-Ahwasw, kutoka kwa ´Abdullaah, ambaye amesema:
”Inatosha kwa mtu kuwa mwongo kuzungumzia kila anachokisikia.”
76 – Abu Bakr ametukhabarisha: Yaziyd bin Haaruun ametukhabarisha: Hammaad bin Salamah ametukhabarisha, kutoka kwa Abu Ja´far al-Khatmiy, ambaye ameeleza kwamba babu yake ´Umayr bin Habiyb aliwausia wanawe na kusema:
“Jihadharini na kukaa pamoja na wapumbavu. Kwani hakika kukaa na wapumbavu ni ugonjwa.”
77 – al-Huutwiy ametukhabarisha: Yahyaa bin Swaalih ametukhabarisha, kutoka kwa ´Abdul-Malik bin Mudrik al-Kalaa-iy, kutoka kwa baba yake, kutoka kwa Abud-Dardaa’, ambaye amesema:
“Katika uelewa wa mtu ni pamoja na anatembea, anaingia na anaotoka pamoja na wanazuoni.”
78 – Ibn Numayr ametukhabarisha: Abu Mu´aawiyah na Ibn Fudhayl wametukhabarisha: al-A´mash ametukhabarisha, kutoka kwa ´Umaarah, kutoka kwa Abul-Ahwasw, ambaye amesimulia kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
”Jizowezeni kheri. Kwani hakika kheri inafanywa kwa kuizowea.”
[1] al-Bukhaariy (2475) na Muslim (57).
[2] Muslim (5) na Abu Daawuud (4992).
- Muhusika: Imaam Abu Bakr Ahmad bin Abiy ´Aaswim ash-Shaybaaniy (a.f.k. 287)
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Kitaab-uz-Zuhd, uk. 19-20
- Imechapishwa: 29/06/2025

Muhusika: Imaam Abu Bakr Ahmad bin Abiy ´Aaswim ash-Shaybaaniy (a.f.k. 287)
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Kitaab-uz-Zuhd, uk. 19-20
Imechapishwa: 29/06/2025
https://firqatunnajia.com/09-kukaa-na-wapumbavu-ni-ugonjwa/