62 – Abu Twaalib al-Jurjaaniy ametukhabarisha: Muhammad bin Salamah ametukhabarisha, kutoka kwa Muhammad bin Ishaaq, kutoka kwa ´Abdullaah bin Abiy Najiyh, kutoka kwa Mujaahid, kutoka kwa Umm Mubashshir bint al-Baraa’ bin Ma´ruur, ambaye amesimulia kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alisema kuwaambia Maswahabah zake:

“Je, nisikujulishe watu ambao ni wabora zaidi?” Wakasema: ”Ndio, ee Mtume wa Allaah.” Akasema: “Mtu anayejikinga na shari za watu.”[1]

63 – Husayn ametukhabarisha: Ibn-ul-Mubaarak ametukhabarisha: Ma´mar ametukhabarisha, kutoka wa az-Zuhriy, kutoka kwa Abu Salamah, kutoka kwa Abu Hurayrah, ambaye ameeleza kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Yeyote ambaye anamwamini Allaah na siku ya Mwisho basi aseme yenye kheri au anyamaze.”[2]

64 – Abu Bakr ametukhabarisha: Abu Usaamah ametukhabarisha, kutoka kwa Mis´ar, kutoka kwa Abu Huswayn, ambaye amesimulia kuwa ´Abdullaah amesema:

“Jihadhari na maneno ya kubwabwaja. Inatosha kusema kile kinachohitajika.”

65 – Abu Bakr ametukhabarisha: Abu Usaamah ametukhabarisha: Sufyaan ametukhabarisha, kutoka kwa Abul-Muhajjal, kutoka kwa Ibn ´Imraan bin Hittwaan, kutoka kwa baba yake, ambaye ameeleza kwamba Abu Dharr amesema:

“Ni bora kuwa peke yako kuliko kuwa na rafiki mbaya.”

66 – Ibn Numayr ametukhabarisha: Qabiysah bin ´Uqbah ametukhabarisha, kutoka kwa Sufyaan, kutoka kwa al-A´mash, kutoka kwa Mujaahid, kutoka kwa ´Abdur-Rahmaan bin Abiy Laylaa, kutoka kwa Abu Dharr, aliyesema:

“Natamani ningekuwa mti uliotafunwa.”

67 – ´Uthmaan bin Abiy Shaybah ametukhabarisha: ´Abdullaah bin Idriys ametukhabarisha, kutoka kwa Maalik, kutoka kwa Abu Swakhrah, kutoka kwa Ziyaad bin Hudayr, ambaye amesema:

“Natamani ningekuwa ndani ya uzio wa chuma na nipate kile ninachohitaji. Siwazungumzishi watu nao hawanizungumzishi mpaka pale nitapokutana na Allaah (Tabaarak wa Ta´ala).”

68 – Abu Bakr ametukhabarisha: Abu Mu´aawiyah ametukhabarisha, kutoka kwa al-Hasan bin Saalim bin Abiyl-Ja´d, kutoka kwa baba yake, kutoka kwa Abu Dharr, ambaye amesema:

“Nina nini mimi na watu? Nimewaachia vyeupe vyao na vyamanjano vyao.”

69 – Abu Bakr ametukhabarisha: ´Abdullaah bin Numayr ametukhabarisha: Raziyn al-Juhaniy ametukhabarisha: Abur-Raqaad ametukhabarisha:

“Nilikuwa mvulana nilipotoka na mmiliki wangu. Nikaletwa mbele ya Hudhayfah ambaye nilimsikia akisema: “Katika zama za Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ilikuwa mtu anaweza kuzungumza neno na akawa kwa neno hilo mnafiki. Leo namsikia mmoja wenu akisema hivyo hivyo mara nne kwenye kikao kimoja.”

70 – Abu Bakr ametukhabarisha: Mu´aawiyah bin Hishaam ametukhabarisha, kutoka kwa Sufyaan, kutoka kwa al-Haarith al-Azdiy, kutoka kwa Ibn-ul-Hanafiyyah, ambaye amesema:

“Allaah amrehemu mtu ambaye anauchunga ulimi wake, akaitajirisha nafsi yake na akakaa nyumbani kwake. Anapata kile anachotegemea.”

[1] Swahiyh kwa mujibu wa al-Albaaniy katika “Swahiyh-ut-Targhiyb wat-Tarhiyb” (2737).

[2] al-Bukhaariy (6018) na Muslim (47).

  • Muhusika: Imaam Abu Bakr Ahmad bin Abiy ´Aaswim ash-Shaybaaniy (a.f.k. 287)
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Kitaab-uz-Zuhd, uk. 17-19
  • Imechapishwa: 29/06/2025