09. Kuadhibiwa ndani ya kaburi kwa sababu ya kunywa pombe

E- Kuadhibiwa ndani kaburi kwa ajili ya kunywa pombe

Katika zama za Salaf alikuweko bwana mmoja ambaye alikuwa anakunywa mvinyo ambao kuna maoni tofauti juu ya uhalali wake. Akauliwa akiwa shahidi ambapo mtu mmoja akamuota usingizini akiwa amevaa koti la rangi ya kijani. Akaambiwa:

“Allaah amekufanya kitu gani?” Akasema: “Unafikiri atamfanya nini ambaye amekufa shahidi? Amenisamehe na akaniingiza Peponi.” Alipogeuka nikaona alama ya kipigo cha bakora mgongoni mwake. Nikasema: “Simama!” Akasema: “Umeona?” Nikaitika: “Ndio.” Akasema: “Mwambie baba yangu: “Ee mla maangamivu! Ule mvinyo ambao mimi na wewe tulikuwa tukinywa usiunywe! Mpaka mimi ambaye nimekufa hali ya kuwa shahidi sijasalimika kupigwa bakora kwa sababu yake.”[1]

[1] Ibn Abiyd-Dunyaa katika ”Dhamm-ul-Muskir”, uk. 82

  • Mhusika: Imaam Zayn-ud-Diyn bin Rajab al-Hanbaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Dhamm-ul-Khamr, uk. 20-21
  • Imechapishwa: 26/07/2020