Swali 9: Ni ipi hukumu kwa yule anayemtukana Allaah, Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na anatukana dini, kisha anaponasihiwa katika jambo hili anajitetea kwa kusema anatafuta riziki na mahitaji ya maisha? Je, mtu huyu ni kafiri au ni muislamu anayehitaji kuadhibiwa na kupewa adhabu kali? Je, katika mazingira haya inaweza kusemwa kwamba kuna tofauti kati ya tusi na mtukanaji?
Jibu: Sielewi maana ya kujitetea kwa kutafuta riziki na mahitaji ya maisha. Ikiwa makusudio ni kwamba anapoambiwa ajifunze dini anajitetea kwa kusema anatafuta riziki, basi kujifunza ni jambo jingine. Lakini sasa tunamhukumu kwa sababu ya tusi hili na tunasema:
“Mwenye kumtukana Allaah au kumtukana Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) au kutukana dini, basi hili ni ukafiri kwa mujibu wa makubaliano ya Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa’ah.”
Ama kuhusu suala la kujitetea kwa kutafuta riziki na mahitaji ya maisha pale anapoambiwa ajifunze dini yake, huu ni uongo. Ni wajibu kwa mtu kujifunza yale ambayo ataendesha kwayo dini yake, kama ambavyo anatafuta riziki na mahitaji yake. Ni lazima pia ajifunze dini yake ili imani yake iwe sahihi, ajifunze kile ambacho Allaah amemfaradhishia kuhusu ´Aqiydah sahihi, kwamba Allaah anastahiki kuabudiwa peke Yake na ajifunze katika twahara, swalah, swawm, zakaah na hajj. Kwa hiyo kujitetea huku hakuna msingi wowote. Ikiwa mtu anapoambiwa: “Jifunze yale ambayo Allaah amekufaradhishia, waulize wanazuoni kuhusu maneno yako kama ni ukafiri au si ukafiri” anajitetea kwa kusema anatafuta riziki, ni uwongo. Kutafuta riziki hakumzuii mtu kujifunza dini yake, kujifunza ikiwa maneno fulani ni ya kikafiri au kuuliza kuhusu hilo, kwa sababu kutafuta riziki hakuchukui muda mwingi na kuna muda mrefu wa kufanya shughuli hiyo.
Aidha hakuna tofauti kati ya tusi na mtukanaji. Tunachosema ni kwamba yeyote anayemtukana Allaah, Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) au dini Yake, basi huyo ni kafiri na mtukanaji ni kafiri, kwani hana udhuru katika hili. Anayeweza kupewa udhuru ni yule ambaye maneno yake yana utata. Kwa hivyo katika hali hii tunatofautisha kati ya maneno na msemaji wake. Kwa mfano mtu akizungumza maneno yenye utata au maneno yanayoweza kuwa na udhuru, basi hapa tunasema:
“Maneno ni ya kikafiri, lakini msemaji wake hakufurishwi isipokuwa baada ya kutimia masharti na kuondoka kwa vikwazo na baada ya kusimamishiwa hoja.”
Lakini mwenye kumtukana Allaah, Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) au dini Yake, hili ni jambo dhahiri na hakuna shaka katika ukafiri wake.
- Muhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: As-ilah wa Ajwibah fiy-Iymaan wal-Kufr, uk. 26-28
- Imechapishwa: 05/01/2026

Muhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: As-ilah wa Ajwibah fiy-Iymaan wal-Kufr, uk. 26-28
Imechapishwa: 05/01/2026
https://firqatunnajia.com/09-hukumu-ya-kumtukana-allaah-na-mtume-wake-ii/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window) Telegram
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window) WhatsApp
- Click to print (Opens in new window) Print
- Click to email a link to a friend (Opens in new window) Email
- Click to share on Facebook (Opens in new window) Facebook
- Click to share on X (Opens in new window) X
- Click to share on Pocket (Opens in new window) Pocket