Mtunzi (Rahimahu Allaah) amesema:
“Unakuwa ni wajibu wakati wa hadathi… “
Kitu kinachowajibisha kutawadha ni hadathi. Allaah (Ta´ala) amesema:
يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا إِذَا قُمْتُمْ إِلَى الصَّلَاةِ فَاغْسِلُوا وُجُوهَكُمْ وَأَيْدِيَكُمْ إِلَى الْمَرَافِقِ وَامْسَحُوا بِرُؤُوسِكُمْ وَأَرْجُلَكُمْ إِلَى الْكَعْبَيْنِ
“Enyi mlioamini! Mnaposimama kwa ajili ya swalah, basi osheni nyuso zenu na mikono yenu mpaka kwenye visugudi na panguseni kwa [kupaka maji] vichwa vyenu na miguu yenu hadi vifundoni.”[1]
Hii ndio Aayah ya wudhuu´. Wengi katika Salaf wamesema kuhusu maneno Yake (Ta´ala):
إِذَا قُمْتُمْ إِلَى الصَّلَاةِ
“Mnaposimama kwa ajili ya swalah.”
“Ilihali ni wenye hadathi.”[2]
Ni lazima mjitwahirishe.
al-Bukhaariy na Muslim wamepokea kupitia kwa Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ´anh) ambaye ameeleza kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Allaah hakubali swalah ya mmoja wenu pindi anapopata hadathi mpaka atawadhe.”
Kuna bwana mmoja kutoka Hadhwramawt aliseama:
“Hadathi ni kitu gani, ee Abu Hurayrah?” Akasema:
“Kutokwa na upepo kwa sauti au pasi na sauti.”
Pindi upepo ukitoka kwa sauti huitwa (ضُراط) au upepo ukitoka pasi na sauti huitwa (فُساَءٌ). Ikiwa kutokwa na upepo kunazingatiwa ni hadathi basi ni lazima kwa mtu atawadhe. Miongoni mwa hayo ni haja kubwa na ndogo ambavyo vina haki zaidi ya kuzingatiwa kuwa ni hadathi. Muslim amepokea katika “as-Swahiyh” yake kupitia kwa ´Abdullaah bin ´Umar (Radhiya Allaahu ´anhumaa) ambaye amesimulia kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema: “Nimemsikia Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akisema:
“Allaah hakubali swalah pasi na twahara wala swadaqah yenye kutokana na kukhini ngawira.”
Wudhuu´ ni kule kutumia maji katika viungo vinne baada ya kunuia. Viungo vinne ni uso, mikono miwili, kichwa na miguu. Viungo vinavyooshwa mara tatu ni uso, mikono na miguu. Kiungo kimoja kinapanguswa juu yake ambacho ni kichwa. Aidha ni lazima pia kupangilia kati yavyo na kiungo kimoja kisiwahi kukauka kabla ya kuoshwa cha kufuata, kama itavyokuja huko mbele.
[1] 05:06
[2] Tafsiyr Ibn Kathiyr (02/22).
- Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
- Mfasiri: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Sharh Shuruwt-is-Swalaah, uk. 18-19
- Imechapishwa: 07/12/2021

Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
Mfasiri: Firqatunnajia.com
Marejeo: Sharh Shuruwt-is-Swalaah, uk. 18-19
Imechapishwa: 07/12/2021
https://firqatunnajia.com/09-hapa-ndipo-inalazimika-kutawadha/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)